Mwanamke aliyetambulika kwa jina la Wande Emanuel (30) mkazi wa kijiji cha Sibwesa Wilayani Tanganyika Mkoa wa Katavi, amekutwa amejinyonga kwa kutumia kipande cha kitenge chake baada ya kudaiwa kumjeruhi kwa kumkata kichwani na kitu chenye ncha kali Mume wake anayefahamika kwa majina ya Dotto Enosi (35).
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Machi 20, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ACP Ali Makame Hamad amesema tukio hilo limetokea Machi 18, 2022 majira ya saa saa sita usiku katika kitongoji cha Kamlenga, kijiji cha Sibwesa.
ACP Hamad amesema chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kifamilia uliosababishwa na shughuli za kilimo, ambapo imedaiwa kuwa Mwanamke alikuwa hataki kwenda shamba kulima hali iliyosababisha kutokea ugomvi huo uliomfanya Mwanamke huyo kumvizia Mume wake akiwa amelala na kumkata na kitu chenye ncha kali kichwani.
Chanzo - Site Digital Media
Social Plugin