Na Costantine Mathias - Malunde 1 blog Bariadi.
Watu saba wamepoteza maisha huku wengine wanane wakujeruhiwa kufuatia ajali iliyotokea eneo la Kidulya nje kidogo ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu, ajali iliyohusisha Lori, Trekta na bajaji.
Imeelezwa kuwa lori lenye namba za usajili T 172 AUP lililokuwa na tela lenye namba za usajili T 471 ABT lilikuwa limepakiwa matofali likitokea barabara ya Luguru kwenda mjini Bariadi liligongana uso kwa uso na bajaji baada ya kutaka kulipita trekta na kusababisha vifo mara baada ya bajaji kuungua moto.
Akithibitiaha kupokea majeruhi na miili ya marehemu Kaimu Mganga Mkuu halmashauri ya mji wa Bariadi Marco Igenge amesema ajali hiyo imetokea marchi 27 (saa 1:00 jioni) na kuongeza kuwa walipokea majeruhi na miili majira ya saa mbili kasoro usiku na kwamba hali za majeruhi zinaendelea vizuri.
Nao baadhi ya majeruhi akiwemo Manjale Kasule wamesema walikuwa nyuma ya tera lililokuwa likikokotwa na Lori na ndani lilikuwa na matofali na baada ya Lori kukwepa trekta na kuigonga bajaji trekta lilianguka na matofali yakawafunika huku mashuhuda wa ajali hiyo wakisema chanzo kikubwa cha ajali ni trekta.
Ajali hii iliyohusisha vyombo vitatu vya moto imegharimu maisha ya nguvu kazi ya taifa na kusababisha majeraha ya kwa waganga wa tukio hilo.