ASKOFU KILAINI ATAJA ADUI WA MAENDELEO KAGERA

Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba Mhashamu Methodius Kilaini

Na Mbuke Shilagi - Kagera

Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba Mhashamu Methodius Kilaini amesema kuwa wivu, chuki, utengano na mfarakano ndiye adui mkubwa wa maendeleo ya Wanakagera.

Askofu Kilaini ameyasema hayo katika Misa ya Jubilei ya Dhahabu ya miaka 50 ya upadre wake, iliyofanyika katika Kanisa Kuu Katoliki Jimbo la Bukoba, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini na serikali, wakiongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Mpango.

Ameongeza kuwa umoja na mshikamano unapopungua katika mioyo ya watu inasababisha kurudisha nyuma maendeleo na kuwa maskini kimwili na kiroho.

Amewataka wananchi kuachana na masuala yote yanayokwamisha maendeleo na badala yake  wawe wamoja ili kuhakikisha maendeleo ya Wanakagera yanapanda kiwango na kuwa juu kiuchumi.

Askofu Kilaini amezaliwa tarehe 30 Machi 1948 huko Lukindo kata Katoma wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, na kupata Upadre mwaka 1972 huko Roma nchini Italia, wakati huo akiwa na umri wa miaka 24. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post