Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya fedha na mipango Lawrence Mafuru akiongea kwenye halfa ya uzinduzi wa Bodi ya PSPTB leo Jijini Dodoma
Baadhi ya washiriki katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya wakurugenzi na wataalam wa ununuzi na ugavi iliyofanyika leo Jijini Dodoma.
Na Dotto Kwilasa,Malunde 1 Blog-DODOMA.
NAIBU Katibu mkuu,Wizara ya fedha na mipango Lawrence Mafuru amezindua Bodi ya Wakurugenzi na wataalam wa ununuzi na ugavi (PSPTB) huku akiwataka Maafisa masuhuri wa Serikali kuzingatia waraka wa manunuzi ili kuongeza nidhamu katika kada hiyo.
Hayo yamejiri leo jijini hapa
katika halfa fupi ya uzinduzi wa Bodi ya hiyo ambapo ametoa wito kwa bodi hiyo kwenda kusimamia kwa ukamilifu Sheria za manunuzi ya umma ili kukidhi kaguzi mbalimbali ambazo bado zinaonyesha haziko sawa kutokana na baadhi ya wataalam hao kukiuka maadili ya taaluma yao.
Akiongea kwa niaba ya Waziri wa fedha Dkt.Mwigulu Nchemba ,Naibu Katibu Mkuu huyo ametoa maelekezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya wataalam wa ununuzi na ugavi na
wajumbe wake kuchukua hatua za kinidhamu kwa wanaokiuka taratibu zilizowekwa na kuwataka kuzingatia miiko ya PSPTB.
"Wadau wa ununuzi na ugavi wana matumaini makubwa kutoka kwenu, nyie ndio mtatoa dira chanya katika kutekeleza majuku yao na hii inajumuisha usimamizi wa maadili na mienendo ya Wataalam,
Uhuwishwaji na utengenezaji wa mitaala unaozingatia umahili wa kitaaluma na mahitaji ya soko ni muhimu pia uandaaji na usimamiaji wa miongozo mbalimbali inayohusu taaluma izingatiwe ipasavyo ikiwa ni pamona na kufanya tafiti mbalimbali zinazohusu taaluma hii,"ameeleza
Pamoja na hayo Mafuru ameitaka Bodi hiyo kutoa majibu kwa changamoto zinazojitokeza kwenye kada hiyo, utoaji wa mafunzo endelevu kwa wataalam na wadau wengine kwenye mnyororo wa ununuzi na ugavi ili kuongeza tija katika utendaji.
"Mkafanye kazi za ushauri zinazohusu taaluma ya ununuzi na ugavi na kusimamia vyema matumizi ya tehama na mifumo ya kielectroniki katika shughuli za kusajili wataalam,"amesema na kuongeza;
Nawahakikishia kuwa serikali kupitia Wizara hii itawapa ushirikiano kwa hatua zinazolenga kuondoa kabisa uzembe na ukiukwaji wa maadili katika fani ya ununuzi na ugavi kwani pesa nyingi za serikali,"amesisitiza
Sambamba na hayo ametumia nafasi hiyo kuhakikisha waajiri wote wanatoa ushirikiano kwa Bodi hiyo, hasa linapokuja suala la usimamizi wa maadili kwa wataalam waliosajiliwa na Bodi.
Amesema,waajiri wanaaswa kutoa taarifa kwenye Bodi zinazohusiana na ukiukwaji wa maadili kwa wataalam, ili hatua stahiki zichukuliwe kwani hakuna ufanisi bila maadili na weledi na kusisitiza kuwa wanapaswa kukikisha wanaajiri watumishi wenye sifa stahiki zinazotambuliwa na sharia ya PSPTB.
"Zingatieni mahitaji yaliyopo kwenye Waraka wa Maendeleo ya Utumishi Na. 3 wa mwaka 2015 wa kada zilizopo chini ya Wizara ya Fedha na hakikisheni kuwa wafanyakazi wanafanya kazi katika mazingira yenye utulivu wa kutosha ili waweze kutoa tija katika utendaji wao,"amesisitiza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PSPTB,Jacob Kibona ameeleza kuwa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi, imepewa jukumu la kusimamia misingi ya taaluma ya ununuzi na ugavi na mienendo ya wataalamu wake hivyo ina wajibu wa kuzalisha wataalam wenye weledi na uwezo wa kutekeleza majukumu yao.
"Bodi hii itasimamia na kuimarisha taaluma ya ununuzi na ugavi sambamba na kuongeza nguvu ya kupambana na vitendo vyote vinavyokinzana na maadili ya kitaaluma ya ununuzi na ugavi kama ubadhirifu wa mali, rushwa na ukiukwaji wa taratibu za ununuzi na ugavi,"amesema.
Ameeleza kuwa kufanya kazi kwa bidii ni kipaumbele cha Bodi hiyo na kwamba wataalam waliopo wanapimwa Kwa kigezo cha uaminifu ili kufanya utafiti wa kitaalamu ambao umesimama kwa sababu ya kukosa fedha, uendeshaji wa taratibu za maadili ya wataalamu wa ununuzi na ugavi,utengenezaji wa mitaala ya kitaaluma, kuandaa agenda za utafiti (Research Agenda).
Social Plugin