Mkurugenzi wa Afrika wa Nuru kwa Mataifa Mchungaji Dkt. Lau Tumusiime aliyekaa wa kwanza kutoka kulia ambae ni mwaandaji wa mkutano mkubwa wa Injili wa mhubiri wa kimataifa , Dana Morey toka nchini Marekani alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mjini Kahama kuhusu mkutano huo ulioanza jana mjini hapa katika Manispaa ya Kahama na aliyesimama ni mkalimani wake. Picha na Patrick Mabula.
Mchungaji Dkt. Lau Tumusiime wa kwanza kulia mwaandaaji wa mkutano wa mkubwa wa Injili kwa kushirikiana na makanisa ya Umoja wa Kipetekoste wilaya ya Kahama zaidi ya 200 ulioanza mjini Kahama na Mhubili wa Kimataifa , Dana Morey toka nchini Marekani unafanyika katika uwanja wa Magufuli , Manispaa ya Kahama , wa katikati ni Mchungaji Sixbert mratibu wa mkutano na mwisho kushoto ni Katibu wa Umoja wa makanisa (CPCT) Emmanuel Majura.
Na Patrick Mabula , Kahama.
Umoja wa makanisa ya Kipendekoste wilayani Kahama (CPCT) wa kushirikiana na mhubiri wa kimataifa Mwijilisti Dana Morey wa kanisa la Miracle Gospel Harvest (MGH) kutoka nchini Marekani wameanza mkutano mkubwa wa kuombea taifa dhidi ya mauaji na ukatili wa wanawake na watoto mjini Kahama.
Mkutano huo wa siku tatu ulianza jana katika kiwanja cha Magufuli , Manispaa ya Kahama unategemea kuhitimishwa kesho siku ya jumapili ambapo pamoja na kuliombea taifa pia utakuwa wa maombi mbalimbali pamoja na wenye shida mbalimbali wataombea.
Akiongea na Waandishi wa habari mjini Kahama , Mkurugenzi wa Afrika wa Nuru kwa Mataifa ,Mchungaji Lau Tumusiime alisema Tanzania ni nchi nzuri kwa kutumia mkutano huo kuombea amani , pamoja na mauaji na ukatili wa kijinsia kwa watoto na wananawake ili Mungu atuepushe na mabaya hayo.
Mchungaji Tumusiime alisema shetani huwa hafurahii maendeleo yoyote yanayotokea kwa hiyo kwa kutumia Injili na maombi katika mkutano huo wataikabidhi nchi ya Tanzania kwenye mamlaka ya Mungu ili matukio hayo mabaya yaweze kukoma miongoni mwa jamii.
Alisema umoja wa makanisa wameamua kufanya mkutano huo kumuomba Mungu aliepushe taifa na matukio hayo kwa sababu huwezi kumuondoa shetani kwa mwili mabadiliko yoyote mema huwa yanafanywa na Mungu mwenyewe.
Mchungaji Tumusiime alisema Tanzania na watu wake ni wazuri sana kutokana na kuwa wanaishi vizuri na nchi zote majirani wao Afrika na Mashariki na Kati na ndiyo wapo hapo kuwaletea Habari Njema ya Injili.
Alisema ni wakati mzuri watu wote bila kujali imani yao wanapaswa kufika kwa Bwana na kuona nguvu ya Mungu anavyowajali nao wachungaji na wainjilisti wanavyowajali na ndiyo maana kabla ya mkuatano walianza na mambo ya kijamii kwa kufanya usafi wa mazingira katika Manispaa ya Kahama na kugawa msaada wa mipira 200 katika shule za msingi na kusaidia Magereza misaada ya kibinadamu.
Social Plugin