David Bennett akiwa hospitali.
***
David Bennett aliyekuwa binadamu wa kwanza Duniani kupandikizwa moyo wa nguruwe amefariki dunia baada ya kuishi kwa miezi miwili akiwa na moyo wa nguruwe.
David (57) aliyekuwa na maradhi ya moyo, alifanyiwa upasuaji Januari 7,2022 nchini Marekani katika hospitali ya University of Maryland Medical Center.
Baada ya kupandikizwa moyo wa nguruwe alijumuika na familia yake baada ya wiki kadhaa na kutazama fainali za Super Bowl pamoja, na hali yake ilianza kubadilika siku kadhaa zilizopita mpaka umauti ulimpofika Machi 8 mwaka huu.
Social Plugin