Watanzania wengi wamekuwa wakiumizwa na changamoto za vijana wao kuijiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya na kujikuta wanapoteza malengo yao ya kimaisha kama vile kupata elimu, kuwa na maisha mazuri, kuwa na familia bora na kujikuta wanaangukia kwenye utegemezi mkubwa badala ya wao kutegemewa.
Nikiwa mshauri na mwandishi mbobezi wa masuala ya dawa za kulevya na uhalifu Afrika nieleze kwa ufupi juu ya changamoto hii.
Matumizi ya dawa za kulevya holela ni kinyume na sheria zetu za Nchi ikiwemo sheria ya dawa za kulevya ya Tanzania.
Dawa za kulevya zina athari ya kimwili, kiroho na kiakiri., athari hizo zote uenda kwa pamoja na haziwezi kukuacha salama kama unatumia dawa za kulevya.
Dawa za kulevya zinawekwa kwenye makundi makubwa matatu.
Kundi la kwanza
Vichangamshi. Kundi ili linajumuisha zile dawa za kulevya zenye kuleta uchangamshi zenye asili ya mmea wa cocaine, hapa tunazungumzia cocaine yenyewe, ambapo mtu anapotumia muda wote atakuwa mchangamfu.
Kundi la pili
Vipumbaza, kundi ili ni aina ya dawa za kulevya zenye kupumbaza, yani mtu anapotumia anakuwa legelege, hapa dawa za kulevya zinazohusika ni heroine. Mtumiaji wa kundi ili anapotumia anakuwa anavaa uhusika wa kuishi kwenye Dunia nyingine na kumfanya kulala muda mwingi na kutafuta faraja za muda.
Kundi la tatu
Maruweruwe, kundi ili linajumuisha dawa za kulevya zenye kuleta hisia mbaya ya ujinamizi kama ndoto mbaya na mambo mengine.
Mfano wa kundi ili ni dawa za kulevya aina ya bangi ambapo mtu akivuta anaweza kuona anakimbizwa na panga na mtu mwingine yote hii inasababishwa na maruweruwe.
Haya ndiyo makundi makubwa matatu ya dawa za kulevya japo yapo mengine madogo madogo ambayo yanaweza kutambuliwa na kuingizwa kwenye makundi haya makubwa, mfano matumizi ya dawa za kutengenezwa kienyeji kama petrol au gundi au matumizi ya kiwango cha juu cha dawa za viwandani.
Kimsingi dawa zote zina athari kubwa kwa afya ya binadamu.
Je mtu anayetumia dawa za kulevya anaweza kupona ?
Jibu ni ndiyo mtu anayetumia dawa za kulevya anaweza kupona kabisa na kuacha kutumia dawa za kulevya kwa kupata huduma kwenye vituo vya sober house, ushauri nasaha au kuhudhuria kliniki maalumu za dawa za kulevya.
Kwenye somo langu la pili nitaeleza kwa kina juu tiba hizo kwa leo niishie hapa kwa kusisitiza kuwa usikate tamaa kama una kijana wako ambaye amedumbukia kwenye matumizi ya dawa za kulevya chukua hatua unaweza kumuokoa bila kumnyanyapaa.
Kwa ushauri wasiliana nami kupitia
0754551306
Barua pepe : edwinsoko22@gmail.com
Edwin Soko
Social Plugin