Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DORIYE AWATAKA WATUMISHI NIC KUENDELEZA USHIRIKIANO KAZINI

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw.Elirehema Doriye akipata picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa NIC mara baada ya kukutana nje ya kazi kwaajili ya kufanya mazoezi kwa pamoja na kujenga mahusiano mazuri kazini. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw.Elirehema Doriye akipata picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa NIC mara baada ya kukutana nje ya kazi kwaajili ya kufanya mazoezi kwa pamoja na kujenga mahusiano mazuri kazini. Baadhi ya watumishi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) wakicheza michezo mbalimbali mara baada ya kukutana nje ya kazi kwaajili ya kufanya mazoezi kwa pamoja na kujenga mahusiano mazuri kazini. Baadhi ya watumishi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) wakicheza michezo mbalimbali mara baada ya kukutana nje ya kazi kwaajili ya kufanya mazoezi kwa pamoja na kujenga mahusiano mazuri kazini. Baadhi ya watumishi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) wakicheza michezo mbalimbali mara baada ya kukutana nje ya kazi kwaajili ya kufanya mazoezi kwa pamoja na kujenga mahusiano mazuri kazini. Baadhi ya watumishi wa Shirika la Bima la Taifa wakicheza mchezo wa kuvuta kamba mara baada ya kukutana nje ya kazi kwaajili ya kufanya mazoezi kwa pamoja na kujenga mahusiano mazuri kazini.

Meneja wa Rasilimali Watu na Utawala NIC, Bi.Veneranda Mpaze akizungumza na watumishi wa NIC mara baada ya kukutana nje ya kazi kwaajili ya kufanya mazoezi kwa pamoja na kujenga mahusiano mazuri kazini.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WATUMISHI wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) wamekutana pamoja nje ya eneo la kazi kujadili ni namna gani wanaweza kuendeleza ushirikiano katika kazi ili wateja wao waweze kufurahia huduma zinazotolewa na Shirika hilokwa kupata huduma iliyobora zaidi.

Akizungumza katika siku hiyo Muhimu ambayo wameiandaa kwa kuipa jina la "NIC Cooperate Day" Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw.Elirehema Doriye amesema wanatakiwa kuwa Team Work kitu ambacho wanatakiwa kukijenga wakiwa ndani nje ya makazini mwao ili huduma wanayoitoa iwe bora kutegemeana na ushirikiano wanaoutoa kwa wenzao.

"Tunapokuwa na mahusino mazuri sisi maanake pia tunaweza kusaidiana, kushauriana lakini kwa pamoja tunaweza kuweka mawazo ambayo yanaweza kuleta chachu ya ubunifu". Amesema

Amesema siku hii iwe mwanzo wa namna wanavyofungua mawasiliano katikati yao kwasababu dhumuni kubwa la kukutana na kushiriki katika shugghuli mbalimbali ili waweze pia kuwasiliana.

Kwa upande wake Meneja wa Rasilimali Watu na Utawala NIC, Bi.Veneranda Mpaze amesema wamekutana kwaajili ya kuhamsha afya ya akili na mwili pamoja na kusapoti mpango wa kitaifa wa kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza mahala pa kazi.

Aidha amesema wafanyakazi hutegemeana hivyo kukutana kwao kuna jenga mawasiliano mazuri na kuweza kuwahudumia wateja wao kwa kupata huduma bora.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com