Viongozi mbalimbali wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wamepiga kura kuridhia Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo (DRC), kuwa mwanachama wa Saba wa Jumuiya hiyo.
Viongozi hao wameridhia suala hilo kupitia kura zilizopigwa wakati wa mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao, ukiongozwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Mwezi Disemba mwaka 2021, wakuu wa Jumuiya hiyo walipokea ripoti ya uhakiki wa utayari wa DRC kujiunga na EAC na kuwataka mawaziri wa Jumuiya hiyo kuharakisha mchakato wa majadiliano ya mkataba ili kuiwezesha DRC kuwa mwanachama na kuiwasilisha mapema mwaka wa 2022 wakati wa mkutano wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo.
DRC ikiwa nchi ya saba kujiunga na Jumuiya hii, kwa sasa ndiyo nchi inyoongoza kwa idadi kubwa ya watu ndani ya nchi zilizopo EAC, ikiwa na watu takribani Milioni 92 jambo litakalopanua mzunguko wa biashara na upatikanaji wa masoko ya bidhaa zinazozalishwa ndani ya Jumuiya.
Lakini pia Tanzania itanufaika hasa katika ukuaji wa matumizi ya bandari, jambo litakalo chochea ukuaji wa uchumi nchini Tanzania pamoja na nchi zilizo ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kiusalama, DRC kudhiriwa kuwa ndani ya EAC itasaidia sana mapambano dhidi ya makundi ya waasi ambao wamekuwa wakitajwa kujificha ndani ya misiti mikubwa DRC na kuzishambulia nchi kama Rwanda na Uganda.
Via EATV
Social Plugin