Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JE UNAFAHAMU BALAA LA BABA WA MABOMU YOTE “VACUUM AU THERMOBARIC”?



Mitambo ya kufyatua roketi ya jeshi la Urusi katika onyesho la ulinzi mjini Moscow mwaka jana

Urusi imekuwa ikishutumiwa kwa kupanga kutumia silaha za aina ya thermobaric - zinazofahamika pia kama mabomu ya vacuum -katika uvamizi wake wa Ukraine.

Silaha hizi ni tata kwasababu husababisha uharibifu mkubwa zaidi kuliko vilipuzi vinavyofahamika vyenye ukubwa sawa na wake, na vina athari mbaya kwa yeyote atakayejipata kwenyeeneo la mlipuko wake.

Je bomu la vacuum linafanya kazi vipi?

Bumu la vacuum, ambalo pia linaitwa bomu la aerosol au kilipuzi cha anga cha mafuta, huwa limeundwa kwa kontena ya mafuta pamoja na vifyatuzi viwili zilizotenganishwa vya vilipuzi.

Bomu hili linaweza kufyatuliwa kama roketi au kudondoshwa kama bomu kutoka kwenye ndege . Wakati linapopiga eneo, kifyatuzi cha kilipuzi hufungua kontena na mchanganyiko mkubwa wa mafuta husambaa kama wingu.

Wingu hili linaweza kupenya kweney mianya yoyote wazi ya jengo au maeneo yaliyolindwa kabisa ambayo yamezibwa kabisa. Kisha kifyatuzi kingine hulipua wingu hil, na kusababisha moto mkubwa, wimbi kubwa la mlipuko na vacuum ambayo hufyonza oksijeni yote inayozingira iliyopo katika eneo zima.


Silaha hiyo inaweza kuharibu majengo, vifaa na kuua au kuwajeruhi watu.


Mabomu haya hutumiwa kwa malengo mbali mbali na hutengenezwa katika ukubwa tofauti - ikiwa ni Pamoja na silaha kwa ajili ya matumizi ya mwanajeshi binafsi kama vile gurunadi na vilipuzi vinavyolipuliwa kwa mkono.


Mabomu haya makubwa yanayofyatuliwa kutoka kwenye ndege pia yametengenezwa, kwa ajili hasa ya kuua wanajeshi au wanaojilinda kwenye mapango na katika mahandaki - athari za silaha hizi huwa mbaya zai katika maeneo yaliyofungwa.


Katika mwaka 2007, Urusi ilifanya majaribio makubwa zaidi ya silaha za Thermobaric, ambazo pia zinaitwa ''Father of all bombs'' (Baba wa mabomu yote) .


Ilitengeneza kilipuzi chenye ukubwa wa tani 44 za bomu la kawaida - na kulifanya kuwa kifaa kikubwa zaidi cha kulipua bomu lisilo la nyuklia duniani.


Kutokana na ubaya wa athari zake, na jinsi yanavyosaidia kujilinda dhidi ya wapinzani ambao huchimba mahandaki ndani ya majengo au mapango ya maficho, mabomu ya vacuum yamekuwa yakitumika katika mazingira ya mijini.


Mabomu haya ni muhimu kutokana na kile kinachoendelea nchini Ukraine, ambako vikosi vya Urusi yanajaribu kuchukua udhibiti wa mji mkuu, Kyiv, na miji mingine muhimu iliyopo mashariki mwa nchi.

Je yanatumiwa katika Ukraine?


Balozi wa Ukraine katika Umoja wa Mataifa Oksana Markarova, ameishutumu Urusi kwa kutumia bomu katika katika uvamizi wake.


Hatahivyo, hakuna uthibitisho rasmi wa madai haya.


Pia kumeripowa na ripoti za kuonekana kwa vilipuzi vya roketi za thermobaric nchini Ukraine katika kipindi cha siku chache zilizopita.

Ni zipi sheria za vita za mambomu ya vacuum ?


Hakunna sheria za kimataifa zinazozuwia matumizi yake, lakini kama nchi inayatumia kuwalenga raia katika makazi ya watu, shule au hospitali , basi inaweza kupatikana na hatia ya uhalifu wa kivita chini ya mkataba wa Heague wa mwaka 2899 na 1907.


Mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu Karim Khan amesema kuwa mahakama yake itachunguza uwezekano wa kutekelezwa kwa uhalifu wa kivita katika Ukraine.

Ni wapi yalikotumika kabla?


Silaha za Thermobaric zilitumika katika Vita ya pili ya dunia , wakati zilipotumiwa kwa mara ya kwanza na jeshi la Ujerumani. Hazikutengenezwa katika maeneo mengi duniani hadi ilipofika miaka ya 1960, wakati Marekani ilipozitumia katika vita vya Vietnam.

Vikosi vya Marekani vilitumia mabomu ya thermobaric dhidi ya Al-Qaeda nchini Afghanistan


Marekani pia iliyatumia katika mwaka 2001 kujaribu kuangamiza maficho ya vikosi vya al-Qaeda forces katika mapango ya milima ya Tora Bora nchini Afghanistan.


Urusi iliyatumia katika vita vya Chechnya katika mwaka 199 na ililaaniwa na shirika la kutete haki za binadamu la Human Rights Watch kwa kufanya hivyo.


Silaha za thermobaric zilizotengenezwa na Urusi ziliripotiwa kutumika katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Syriana utawala wa Bashar al-Assad.

CHANZO - BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com