Wanafunzi wakikimbia katika michezo iliyofanyika shuleni hapo
Afisa Mradi unaolenga kuongeza ubora wa elimu na elimu jumuishi, Rebeca Bugota kutoka kanisa AICT Dayosisi ya Mara na Ukerewe akitoa elimu kwa wanafunzi baada ya michezo.
**
Na Frankius Cleophace Tarime.
KANISA la AICT Dayosisi ya Mara na Ukerewe (MUD) kwa kushirikiana na Taasisi ya Right to Play wamehimiza wazazi na walezi kuendelea kulea watoto wao katika misingi bora ili kuwaandalia maisha ya baadaye.
Hayo yamebainishwa na Afisa Mradi unaolenga kuongeza ubora wa elimu na elimu jumuishi, Rebeca Bugota kutoka kanisa hilo katika hafla ya kufunga michezo ya wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la nne kutoka shule za msingi Nyankoni na Itiryo.
Akizungumzia suala la malezi na makuzi kwa watoto kuanzia miaka 0-8, Rebeca alisema kuwa wazazi wengi wanashindwa kutimiza wajibu wao hususani kwenye suala la malezi bali wanawaachi walimu ili waweze kulea watoto jambo ambalo siyo zuri.
“Mzazi anapaswa kulea mtoto akiwa tumboni na pale anapo zaliwa ni jukumu la Baba na Mama sasa kulea akienda shule akiwa na malezi mazuri hawezi kusumbua walimu pia anapolelewa vyema anaandaliwa mazingira mazuri kwa maisha ya badaye sasa wazazi tujikite kulea watoto wetu wakiwa wadogo”, alisema Rebeca.
Rebeca aliongeza kuwa licha ya kutoea elimu ya kupinga ukatili pia wamekuwa wakitoa elimu juu ya suala la malezi na makuzi na wamekuwa wakitumia michezo mbalimbali ili kufikisha ujumbe uliokusudia jambo ambalo linachangia pia maudhurio shuleni.
Pia alisema kuwa Halmashauri ya wilaya ya Tarime wamefikia shule 15 sawa na wanafunzi 60,000 darasa la awali mpaka darasa la tatu ambao wengi wao wako chini ya miaka Nane kutokana na sera ya elimu.
“Lengo la mashindano haya ni kuihamasisha jamii ya hapa kuona umuhimu wa kuwapa elimu watoto wa kike, ndio maana tuko hapa tukishuhudia michezo mbalimbali kutoka kwa watoto hawa", alisema Rebeca.
Naye mgeni rasmi wa bonanza hilo, Charles Mashauri ambaye ni Mratibu wa mradi huo mkoa wa Mara, amewataka wazazi na watu wote kuthamini elimu kwa mtoto wa kike kwani amekuwa akinyimwa haki zake za msingi.
“Tunapomuelimisha mtoto wa kike anakuwa chachu au kichocheo kwa maendeleo ya jamii, hivyo kwa pamoja tusichoke kuihamasisha jamii,” Mashauri alisistiza.
Mashindano hayo yaliyobeba kaulimbiu inayosema Muelimishe Msichana, kwa Maisha Bora ya Baadaye.
Vilevile Mashindano hayo yamehusisha michezo mbalimbali, ikiwemo mpira wa miguu, riadha na mpira wa pete, huku washindi wakipewa zawadi mbalimbali.
Mashirika mbalimbali yanayo wajibu wa kuendelea kupanza sauti ili kulinda na kutetea haki za watoto hususani kuanzia miaka sifuri mpana nane ili kuwawekea misingi bora ya ukuaji wao.
Mwita Waisiko ni mmoja wa walimu katika shule ya msingi Itiryo alisema kuwa uwepo wa michezo hiyo umeongeza maudhuri kwa wanafunzi nakuomba serikali kuungana na mshirka yanayojitokeza kufikisha elimu ya malezi kwa wazazi hususani maeneo ya vijijini.
Chacha Manko ni Mzazi alisema kuwa changamoto kubwa kwenye jamii ni suala la elimu juu ya umhimu wa malezi na makuzi ya awali ya mtoto hivyo sasa serikali iweze kusisitiza suala la elimu juu ya malezi kuanzia shule za msingi ili watoto waweze kulelewa vyema.