Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ameshirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wa Shinyanga, Kikundi cha Wanawake Laki Moja na Wadau mbalimbali katika Mkoa huo kutoa Msaada kwa wahitaji kuelekea siku ya Wanawake Duniani Machi 8.
Msaada huo umetolewa katika Kituo cha Watoto wenye Ulemavu kilichopo Shule ya Msingi Buhangija, Gereza la Wanawake la Matanda pamoja na Kituo cha Agape kinacholea Wahanga wa Ndoa na Mimba za Utotoni.
Akiwa katika shughuli hiyo Naibu Waziri amewapongeza Wanawake wa Mkoa wa Shinyanga kwa kuguswa na kutoa msaada kwa wahitaji mbalimbali.
Alibainisha kuwa jambo hilo ni ishara tosha kuwa Wanawake wanamuunga mkono Juhudi sa Mheshimiwa Rais katika kuendela kutatua changamoto mbalimbali za wananchi.
Social Plugin