Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KATIBU MKUU UN : GHASIA ZINAONGEZEKA MAPIGANO URUSI NA UKRAINE... HAZIKUBALIKI KABISA, IMETOSHA


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anatarajiwa kutoa wito wa kusitisha mapigano nchini Ukraine.

Mapigano yanavuma kote nchini, kuanzia angani, nchi kavu na baharini. Ni lazima yakome sasa. Makombora na anga ya Urusi yanapiga miji ya Ukraine mchana na usiku. Mji mkuu, Kyiv, umezingirwa na kushambuliwa kutoka pande zote from Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Mapigano yanavuma kote nchini, kuanzia angani, nchi kavu na baharini. Ni lazima yakome sasa. Makombora na anga ya Urusi yanapiga miji ya Ukraine mchana na usiku. Mji mkuu, Kyiv, umezingirwa na kushambuliwa kutoka pande zote.

Pia anatarajiwa kusema kuwa Umoja wa Mataifa una “ushahidi wa kuaminika” Makombora ya Urusi yanalenga maeneo ya makazi, miundombinu muhimu ya raia na maeneo mengine yasiyo ya kijeshi.


“Ghasia hizi zinazoongezeka – ambazo zinasababisha vifo vya raia, wakiwemo watoto – hazikubaliki kabisa. Imetosha. Askari wanapaswa kurejea kwenye kambi zao. Viongozi wanapaswa kuzingatia amani”,Antonio GuterresKatibu Mkuu wa Umja wa Mataifa

Huku hayo yakijiri Ukraine imeomba Muungano wa Ulaya (EU) kuijumuisha kama mwanachama “mara moja”.

Hayo yamesemwa na rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, katika video iliyoshirikishwa mtandaoni Februari 28, 2022 muda mfupi baada ya wajumbe wa Ukraine kuwasili kwenye mpaka na Belarus ili kuanza mazungumzo na wawakilishi wa Urusi.

Mazungumzo ya Kusitisha Mapigano Yaanza Kati ya Russia na Ukraine

Vladimir Medinsky, mkuu wa ujumbe wa Russian, wapili kushoto, na Davyd Arakhamia, kiongozi wa Chama, Bunge la Ukraine, wa tatu kulia, wakihudhuria mkutano wa amani mkoa wa Gomel, Belarus, Jumatatu, Feb. 28, 2022. Sergei Kholodilin/BelTA Pool Photo via AP)

Mazungumzo kati ya Russia na Ukraine yamefanyika katika mpaka wa Belarus Jumatatu wakati ambapo Russia inazidi kutengwa kidiplomasia na kiuchumi siku nne tangu ilipoivamiaUkraine, ikiwa ni shambulizi kubwa kufanyika katika nchi ya Ulaya tangu vita vya pili vya dunia.

Mazungumzo yameanza kwa lengo la kusitisha mapigano na kuondoa wanajeshi wa Russia, ofisi ya rais wa Ukraine imesema.

Hata hivyo operesheni za Russia zimekwenda taratibu tofauti na wengine walivyotarajia.

Mazungumzo yanafanyika katika mpaka na mshirika mkubwa wa Russia, Belarus ambapo kura ya maoni siku ya jumapili iliidhinisha katiba mpya inayoondoa hali ya kutokuwa na nyuklia ya nchi hiyo wakati ambapo jamhuri ya zamani ya Soviet imekuwa uwanja uliotumiwa na wanajeshi wa Russia walioivamia Ukraine.

Majibu ya nchi za magharibi kwa uvamizi huo yamekuwa makubwa wakiweka vikwazo ambavyo zimezuia taasisi kuu za kifedha za Moscow kutoka kwenye masoko ya hisa ya magharibi hatua ambayo imesababisha sarafu ya Russia kushuka kwa asilimia 30 dhidi ya Dola Jumatatu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com