Kiwanda hicho kikiteketea.
KIWANDA cha kutengeneza magodoro na mabati cha GSM kilichopo Mikocheni Jijini Dar, leo kimeteketea kwa moto na kuzua taharuki eneo hilo.
Akizungumza na mwandishi wetu, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kinondoni wa Jeshi hilo, Christina Sunga amesema walipokea taarifa ya moto huo saa kumi na mbili asubuhi ambapo wao kwa kushirikiana na vikosi vingine vya uzimaji moto waliwahi eneo la tukio na kufanikiwa kuudhibiti ingawa baadhi ya mali zilikuwa zimeshateketea.
Kamanda Christina amesema moto huo endapo usingedhibitiwa mapema kulikuwa huenda ungesambaa eneo kubwa na kuhatarisha usalama wa maeneo yote yaliyozunguuka kiwanda hicho.
Kwa upande wake Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Murilo Jumanne Murilo naye alifika eneo la tukio na kumkuta Kamanda wake wa Mkoa wa Kipolisi mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni , RPC Ramadhani Kingai alikuwa ameshafika akiimarisha usalama na vijana wake.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto mkoa wa Kinondoni, Christina Sunga akiwaeleza jambo wanahabari waliokuwa eneo la tukio.
Kamanda Murilo alivishukuriu vikosi vyote vilivyokuwa vikishirikiana kupambana na moto huo ambao mpaka kufikia mida ya saa tano asubuhi ulikuwa ukiendelea kufuka baadhi ya maeneo ya kiwanda hicho.
Kama Murilo amesema katika janga hilo pamoja na kuteketea kwa mali za kiwanda hicho hakuna mtu yeyote aliyeripotiwa kujeruhiwa.
Social Plugin