KUTANA NA BIA HII ILIYOTENGENEZWA KWA KUTUMIA MAJI TAKA



Katika juhudi za kuongeza ufahamu juu ya uwezekano wa kuyabadilisha Majitaka kuwa maji salama kampuni moja inayozalisha bia jijini Stockholm nchini Swaeden imetengeneza bia iliyobatizwa jina la PU: REST kwa kutumia Majitaka yaliyotibiwa (recycled sewage water).

Kampuni hiyo ambayo katika uzalishaji wa bia hiyo wameshirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Mazingira nchini Sweden imedhamiria kupitia kinywaji hicho kuwashawishi wakazi wa nchi hiyo kuwa ‘Maji taka yaliyotibiwa (recycled sewage water)’ ni maji safi na salama kama yanayotoka kwenye mabomba.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Utafiti wa Mazingira nchini Sweden wamesema kuwa changamoto ya watu kutoyaamini majitaka yaliyotibiwa sio ya kiufundi bali ni changamoto ya kisaikolojia na ndio maana wametengeneza bia ili kuwashawishi watu kuyatumia Majitaka yaliyotibiwa.

Kwa sasa PU:REST bia inapatikana pekee katika mgahawa wa New Camegie Brewery’s jijini Stockholm na July 2 itauzwa kwenye migahawa na kwenye matamasha yote nchini Sweden.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم