Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Njombe kwa kushirikiana na wananchi mkoani humo wamefanikiwa kuokoa mwili wa mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 50 kwenye maji ya mto ruhuji ambaye hajafahamika ni mkazi wa eneo gani mwili wake ukiwa umenasa kwenye mawe ya mto huo.
Aidha tukio hilo limetokea kwenye mto eneo la njiapanda ya barabara kuu ya kuingia mjini Njombe na njia ya panda ya barabara ya kutoka Njombe kwenda wilayani Makete.
Akizungumza mara baada ya askari wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoani Njombe wakishirikiana na wananchi kufanikiwa kuutoa mwili wa mtu huyo,kaimu mkuu wa kikosi cha jeshi la zimamoto na uokoaji, Inspector Loth Madauda amesema.
“Mazingira ya eneo ni sehemu ya maporomoko ya maji amabpo alinasa chini ya mawe kwa hiyo inaonekana kama ni mtu aliyetoka kwenye mto mwingine kwa hiyo hatujui chanzo chake katokea wapi”alisema Loth.
Vile vile Inspector Loth Madauda ametoa wito kwa wananchi kuwa makini na maji yanayotiririka.
Social Plugin