Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella
Na Rose Jackson,Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amesema kuwa kupitia halmashauri za Mkoa umeendelea kutenga mapato ya ndani jumla ya shilingi milioni 884.15 kwa kipndi cha Julai hadi Februari 2022 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu 158 katika shule za msingi.
Mongela ameyasema hayo katika Kikao maalum cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Arusha cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kuanzia mwezi Julai 2021 hadi mwezi Februari 2022.
Amesema pia mkoa umetenga shilingi bilioni 1.92 fedha za UVIKO - 19 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 96 ya shule shikizi ili kuondoa adha ya mtoto wanaosoma kutembea umbali mrefu kwa kila halmashauri.
Ameeleza mkoa umetenga kiasi hicho Cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule za msingi ili kuhakikisha wanafunzi qananufaika na elimu bila malipo.
Aidha amesema katika kipindi cha miezi 6 cha utekelezaji wa Ilani jumla ya shule mpya 14 zimeongezeka kutoka shule 823 mwaka 2021 hadi kufikia shule 837 mwezi Februari 2022 ikiwa ni shule za msingi huku upande wa shule za sekondari kukiongezeka kwa shule mpya 17 kutoka shule 252 hadi kufikia shule 269 Februari 2022.
Awali Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dkt. Athuman Kihamia amewakumbusha watendaji walioteuliwa na serikali kuwa waadilifu,wawajibikaji na ambao watazifanya rasilimali kuonyesha matokeo chanya huku wakiyafanya madaraka ya umma kuwa msingi wa maamuzi sambamba na kuwa wafuatiliaji na watathimini katika utekelezaji wa mipango wanayoipanga.
Dkt. Kihamia amewataka watendaji hao kuwa sehemu ya kuthibiti migogoro ya migongano ya kimaslahi ,kudhibiti matumizi mabaya ya ofisi ikiwemo ipotevu wa fedha za umma sambamba na kuwepo mifumo ya kushughulikia kero na malalamiko ya wananchi kwa wakati kwa haki na uadilifu.
Social Plugin