Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge
Na Mbuke Shilagi - Kagera
Hayo yamethibitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge katika kikao cha Kamati ya Amani kilichofanyika katika manispaa ya Bukoba kwa lengo la kuweka mikakati ya kudhibiti vitendo vya mauaji.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa mauaji katika kipindi hicho cha mwaka jana, Wilaya ya Bukoba ni watu 33, Karagwe 28, Muleba 26, Kyerwa 23, Ngara 21, Biharamulo 15 na Missenyi 15.
Pia amesema kuwa katika kipindi cha kuanzia Januari 01 mpaka Machi 07 mwaka huu, watu 31 wameuawa, huku akitaja baadhi ya sababu za mauaji hayo kuwa ni migogoro ya ardhi, migogoro ya kifamilia,ugumu wa maisha pamoja na wivu wa kimapenzi.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Kgera Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba Methodius Kilaini amewataka viongozi wa nyumba zote za ibada kuwa na ofisi za wataalam wa afya ya akili, ili kushauri waumini wao pale wanapopata changamoto katika familia zao.
Aidha amepinga vikali ulevi wa kupindukia ambao umekuwa ukichangia vitendo hivyo viovu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Kgera Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba Methodius Kilaini akizungumza kwenye kikao hicho
Social Plugin