Na Marco Maduhu, Shinyanga
MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobasi Katambi, amefanya mikutano na wajumbe wa halmashauri kuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata, kwa kusikiliza changamoto ambazo zinawakabili wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu, amekutana na wajumbe hao leo kwa nyakati tofauti, kutoka Kata za Chamaguha, Kolandoto, Ibadakuli, Kizumbi, Ngokolo, Ibinzamata, Ndembezi, Kitangili, na Mjini.
Akizungumza wakati wa utatuzi wa kero mbalimbali, ambazo ziliwasilishwa na Madiwani wa Kata husika, na baadhi ya wajumbe wa mkutano huo kwa niaba ya wananchi, alisema kero zote ambazo zimewasilishwa atazitafutia ufumbuzi, kama alivyofanya kwenye utatuzi wa kero zingine hapo awali ambazo zilikuwa changamoto kubwa kwa wananchi.
Aidha, baadhi ya kero ambazo ziliwasilishwa kwenye mkutano huo ilikuwepo ya ukosefu wa huduma za umeme, ubovu wa miundombinu ya barabara, umaliziwaji wa maboma ya Zahanati, upimwaji wa maeneo ya ardhi, upungufu walimu mashuleni, matundu ya vyoo, ukosefu wa maji kwenye baadhi ya maeneo na Ofisi za Chama.
Katambi akizungumza wakati wa utatuzi wa changamoto hizo, alisema suala la upatikanaji wa huduma ya umeme kwenye baadhi ya maeneo ambayo hayana litafanyiwa kazi, ambapo hivi karibuni Waziri husika atafanya ziara jimboni humo na kuitatua changamoto hiyo, pamoja nayeye kulibana Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kuongeza kazi ya usambazaji wa huduma hiyo.
Akizungumza changamoto ya upimaji wa maeneo, alisema tayari Manispaa ya Shinyanga alishapewa fedha Sh.milioni 500 kwa ajili ya upimaji maeneo, ambapo kuna fedha zingine zitakuja na wananchi wataendelea kupimiwa maeneo yao.
Alisema kwa upande wa ubovu wa miundombinu ya barabara, ataendelea kulifanyia kazi, kama alivyofanya hapo awali kwenye baadhi ya maeneo korofi ambapo alitengeneza barabara, madaraja na makalavati.
Kwa upande wa kumalizia ujenzi wa maboma ya Zahanati, alisema tayari kuna fedha zimeshatengwa kwa ajili ya kumalizia maboma hayo katika bajeti ya mwaka wa fedha (2022-2023),huku akibainisha changamoto zote lazima atazitatua.
Pia alizungumzia upande wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege, Stendi ya Mabasi ya kisasa, eneo la maegesho ya Magari, na Soko la kisasa, kuwa utekelezaji wa ujenzi wa miradi hiyo upo katika mipango mizuri na itakapokamilika itaanza kujengwa rasmi.
Katika hatua nyingine Katambi, alitoa wito kwa wananchi wajitokezi kwa wingi kuandikishwa katika zoezi la Sensa na Makazi ya watu, ambalo litafanyika Agost mwaka huu, na washiriki kikamilifu kutoa taarifa sahihi ili Serikali inapokuwa ikipeleka utekelezaji wa miradi ya maendeleo iwe na takwimu za idadi ya watu kamili na kupeleka huduma kwa usahihi.
Katambi aliwashukuru pia viongozi wote wa Chama cha Mapinduzi CCM, kwa kufanya naye kazi kwa ushirikiano, katika kuhakikisha wanatekeleza ilani ya chama hicho kwa vitendo, na kuhudumia wananchi ipasavyo kwa kuwatekelezea miradi mbalimbali ya maendeleo kama walivyo ahidi kipindi cha kampeni kwenye uchaguzi mkuu 2020.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abubakari Mukadam, alimpongeza Mbunge Katambi kwa kuhudhulia mara kwa mara jimboni kwake, na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Pia aliwataka wana CCM kuendelea kuisemea miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa na chama hicho chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassani, ili kuendelea kumpa nguvu na kumtia moyo kuendelea kutafuta fedha za utekelezaji wa miradi hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu, akiwa katika mkutano wa wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Kata.
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Ester Makune, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Abubakari Mkadam, akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Agnes Bashemu, akizungumza kwenye mkutano huo.
Diwani wa Kolandoto Mussa Andrew akiwasilisha taarifa ya Kata kwenye mkutano huo, pamoja na changamoto ambazo zinawakabili wananchi.
Diwani wa Ibadakuli Msabila Malale, akiwasilisha taarifa ya Kata kwenye mkutano huo, pamoja na changamoto ambazo zinawakabili wananchi.
Diwani wa Viti maalum tarafa ya Ibadakuli Zuhura Waziri akizungumza kwenye mkutano huo na kuwasilisha kero za wananchi.
Diwani wa Kitangili Mariam Nyangaka, akiwasilisha taarifa ya Kata kwenye mkutano huo, pamoja na changamoto ambazo zinawakabili wananchi.
Diwani wa Ibinzamata Ezekiel Sabo, akiwasilisha taarifa ya Kata kwenye mkutano huo, pamoja na changamoto ambazo zinawakabili wananchi.
Diwani wa Ndembezi Victor Mmanywa, akiwasilisha taarifa ya Kata kwenye mkutano huo, pamoja na changamoto ambazo zinawakabili wananchi.
Diwani wa Kizumbi Reuben Kitinya, akiwasilisha taarifa ya Kata kwenye mkutano huo, pamoja na changamoto ambazo zinawakabili wananchi.
Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Kata za Kolandoto, Chamaguha na Ibadakuli wakiwa kwenye mkutano huo.
Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Kata za Kolandoto, Chamaguha na Ibadakuli wakiwa kwenye mkutano huo.
Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Kata za Kolandoto, Chamaguha na Ibadakuli wakiwa kwenye mkutano huo.
Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Kata za Kolandoto, Chamaguha na Ibadakuli wakiwa kwenye mkutano huo.
Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Kata za Kizumbi, Ibinzamata, Kitangili, Ngokolo, Ndembezi na Mjini wakiwa kwenye mkutano huo.
Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Kata za Kizumbi, Ibinzamata, Kitangili, Ngokolo, Ndembezi na Mjini wakiwa kwenye mkutano huo.
Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Kata za Kizumbi, Ibinzamata, Kitangili, Ngokolo, Ndembezi na Mjini wakiwa kwenye mkutano huo.
Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Kata za Kizumbi, Ibinzamata, Kitangili, Ngokolo, Ndembezi na Mjini wakiwa kwenye mkutano huo.
Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Kata za Kizumbi, Ibinzamata, Kitangili, Ngokolo, Ndembezi na Mjini wakiwa kwenye mkutano huo.
Viongozi wa CCM wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye mkutano huo.
Viongozi wa CCM wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye mkutano huo.
Na Marco Maduhu, Shinyanga
Via Shinyanga Press Club Blog
Social Plugin