Na Samir Salum
Kupitia taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Machi 05, 2022 na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano (JWTZ) Luteni Kanali Gaudentius Gervas Ilonda amesema kuwa CDF Mabeyo ameamuru Vijana hao wote warejeshwe katika Makambi ya Kujenga Taifa tayari kwa kuanza mafunzo yao mara moja.
Amesema kuwa Mnamo April 12,2021 Jumla ya Vijana wa Kitanzania 854 ambao walikuwa wanaendeea na mafunzo ya kujitolea kwenye Makambi ya JKT, walifukuzwa na kuondolewa makambini na kurejeshwa majumbani mwao kutokana na sababu za kimakosa ya kinidhamu.
"JWTZ imepokea na ina taarifa Kijana mmoja kati ya wale Vijana 854 amefariki na walio hai ni Vijana 853" amesema
Luteni Kanali Ilonda ameeleza kuwa Msamaha ambao Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo ameutoa kwa Vijana hao umetokana baada ya JWTZ kufanya uchunguzi wa kina na utafiti na kujiridhisha na kuonesha kuwa vitendo hivyo vya ukiukwaji wa taratibu za kinidhamu walivyifanya ni kwasababu ya utoto.
"tuache Vijana wapate mafunzo yao ya stadi za maisha ili waje kulitumikia Taifa lao kwa moyo mmoja" Luteni Kanali Gaudentius Gervas Ilonda, Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano (JWTZ)
Social Plugin