Rais Samia akimuapisha Humphrey Polepole kuwa Balozi wa Tanzania katika nchi ya Jamhuri ya Malawi kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 15 Machi, 2022.
**
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi Humphrey Polepole, atawekwa darasani kwanza katika Chuo cha Diplomasia na akimaliza watazungumza.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Machi 15, 2022, Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma, mara baada ya kumuapisha Polepole kuwa Balozi, pamoja na Mkuu wa mkoa wa Njombe, Waziri Kindamba aliowateua jana kushika nyadhifa hizo.
"Mh. Balozi najua baada ya hapa watakuweka darasani kwanza pale Chuo cha Diplomasia, utakapotoka pale kabla hujaenda Malawi nitakutana na wewe kwahiyo tutazungumza kwa urefu," amesema Rais Samia.
Kabla ya uteuzi huo, Polepole alikuwa Mbunge wa Kuteuliwa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Social Plugin