Mwandishi wetu -Mwanza
Kamishina wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mbaraka Samwanza mwishoni mwa wiki iliyopita alifanya ziara ya kikazi Jijini Mwanza na kuthibitisha kuwa, Mwanza ni salama dhidi ya majanga ya moto.
"Nimekagua miundombinu yote ya zimamoto ikiwemo visima vya maji ya zimamoto na kujihakikishia kwamba wakazi wa Jiji la Mwanza wapo salama wao pamoja na mali zao dhidi ya tishio lolote la moto", alisema.
Ziara hiyo ilijumuisha ukaguzi wa visiwa vya maji ya zimamoto kwenye maeneo ya Iseni, kata ya Butimba Jijini Mwanza, Mkolani kata ya Mkolani Jijini Mwanza na kujionea ufanisi wa visima hivyo.
Juma Abdul Mwananchi wa Mkolani amesema hakujua kama jeshi la zimamoto lina miundombinu ya kujazia maji kwenye maeneo mbalimbali, miundombinu hiyo inasadia kupata maji kwa wakati muafaka na ameitaka jamii kuilinda kwa kuwa imasaidia pindi moto unapotokea.