******************
NA EMMANUEL MBATILO
Senegal imefanikiwa kufuzu kombe la Dunia mara baada ya kufanikiwa kuwaondoa Misri kwa mikwaju ya penati baada ya kutoka kwa agg 1-1 kwenye mechi mbili nyumbani na ugenini.
Mechi ya kwanza ambayo ilipigwa nchiini Misri tulishuhudia Misri wakiondoka na ushindi wa bao 1-0 bao ambalo Senegal walijfinga kupitia kwa Saliou Ciss dakika ya 4 ya mchezo.
Katika raundi ya marudiano ambapo Senegal wakiwa nyumbani walipata bao kupitia kwa mshambuliaji wao Boulaya Dia dakika ya 3 ya mchezo na kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi kwenye mechi hiyo na matokeo yakawa agg 1-1.
Baada ya dakika 90 kumalizika ziliongezwa dakika 30 lakini milango yote haikuweza kufunguliwa mpaka hatua ya kupiga penati ikwadia.
Mohammed Salah miongoni mwa wachezaji waliokosa penati kwenye mechezo huo ambapo penati ya Sadio Mane iliwapeka moja kwa moja Senegal kushiriki michuano ya kombe la Dunia nchini Qatar.