SHIRIKA LA PINGOS LAZINDUA RIPOTI YA MABADILIKO YA TABIA NCHI


Afisa wa mabadiliko ya tabia nchi na mazingira kutoka shirika la Pingos Forum, Gedion Sanago akiwa na viongozi wengine katika uzinduzi wa ripoti ya mabadiliko ya tabia nchi na namna ambavyo Wafugaji wanavyokabiliana na madhara yatokanayo na mabadiliko hayo.

Na Rose Jackson,Arusha

Shirika la  Pingos Forum limezindua ripoti ya mabadiliko ya tabia nchi na namna ambavyo wafugaji wanavyokabiliana na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi na namna wanavyohimili majanga ya asili.

Akizungumza katika uzinduzi wa ripoti hiyo uliofanyika katika ofisi za Pingos Forum jijini Arusha afisa wa mabadiliko ya tabia nchi na mazingira kutoka Pingos Forum, Gideon Sanago amesema kuwa ripoti hiyo imefanyika toka mwaka jana ambapo ilifanyika katika vijiji vitano vya wilaya ya Simanjiro.

Amesema kuwa taarifa hiyo imechaguliwa kwa maeneo hayo kukusanya taarifa ambapo vijiji hivyo vitano vinaaksi maeneo mengine ya wafugaji hapa nchini Tanzania ambapo inaangalia suala la wafugaji wa asili wanavyopambana na mabadiliko ya tabia nchi na wanavyohimili majanga ya asili.

Amedai kuwa mabadiliko ya tabia nchi yamekuwa yakiathiri sana maeneo ya Wafugaji hivyjo ripoti hiyo inaangalia namna ambavyo Wafugaji wanavyohimili majanga ya asili ikiwa ni pamoja na ripoti hiyo kuwa na elimu ya asili.

Kwa upande wake ,Nailejileji Tipap kutoka Idara ya Jinsia Maendeleo ya Vijana na Wanawake kutoka shirika la Pingos amesema kuwa ripoti hiyo itasaidia kupata maarifa mengine ambayo yanasaidia jamii.

Naye afisa mifugo kutoka halmashauri ya wilaya ya Simanjiro Dkt.  Swalehe Masaza amesema ripoti hiyo imefanyika Simanjiro na kwamba kikubwa inaelezea majanga makubwa yanayotokana na mabadiliko ya tabia nchi kwa wafugaji wa wilaya ya Simanjiro.

Dkt Masaza amedai kuwa ripoti hiyo inaelezea namna ambavyo wafugaji wanaweza kutumia njia za asili kutibu na kukinga mifugo ikiwa ni pamoja na namna ambavyo wafugaji wanavyoweza kutumia utabiri wa asili.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post