************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KLABU ya Simba imeendelea kutoa dozi ya uhakika kwenye ligi ya NBC mara baada ya leo hii kufanikiwa kuichapa Biashara Fc mabao 3-0 na kuondoka na pointi tatu muhimu.
Simba Sc ilianza kwa kumilika mpira kwa dakika za mwanzo kipindi cha kwanza na kufanikiwa kupata mabao ya mapema kupitia kwa nyota wao Pape Sakho dakika ya 9, Yassin Msamiru dakika ya 14 na Clautos Chama dakika ya 18 ya mchezo.
Katika Msimamo wa ligi NBC mpaka sasa Yanga imeendelea kuwa kileleni mwa ligi kwa pointi 42 ikiwa imecheza mechi 16, wakati mahasimu wao Simba Sc wakiwa wanasalia nafasi ya pili wakijikusanyia pointi 34 wakiwa wameshacheza mechi 16.
Social Plugin