Mratibu wa zao la shairi Kitaifa kutoka TARI bi Salome Munisi akitoa taarifa ya utafiti wa zao la shairi kwa Waandishi wa habari .
Na Rose Jackson - Arusha.
Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Selian inatarajia kuzalisha Tani elfu nane Hadi elfu kumi za shairi kuanzia mwaka 2021 hadi 2025 ili kuweza kukidhi mahitaji halisi yanayohitajika hapa nchini.
Hayo yamebainishwa na mratibu wa zao la shairi kitaifa Salome Munisi wakati akizungumza na waandishi wa habari waliopatiwa mafunzo na COSTECH mara baada ya kutembelea taasisi hiyo kwa lengo la kujifunza habari za matokeo ya utafiti wa kisanyansi kwa vitendo.
Amesema agizo la serikali ni kuhakikisha kuwa uagizwaji wa zao la shairi kutoka nje unapungua hivyo wao wamepewa jukumu la kuzalisha Tani elfu nane Hadi Tani elfu kumi Hadi ifikapo mwaka 2025.
"Mwaka kesho tunatarajia kuvuna Tani kumi na tano na tunategemea mpaka ifikapo mwaka 2025 mvua ikinyesha tunaweza kukidhi mahitaji ambayo tuliambiwa tuzalishe kusudi ni kupunguza changamoto ya uagizwaji wa zao hili kutoka nje ya nchi"aliongeza bi Salome.
Amefafanua kuwa wamekuwa wakifanya utafiti wa zao la shairi ili kupata mbegu bora zinazokidhi mahitaji ya wanunuzi ikiwa ni pamoja na kuwasilisha tafiti zao kwa Wakulima ambao ni wadau wakubwa ili kuongeza tija.
Kwa upande wake Zeda Mtakimwa kutoka kitengo cha ngano TARI Selian amesema kuwa katika kufanya tafiti za ngano Wanazalisha ngano za ukanda wa juu,ngano za Ukanda wa Kati pamoja na ngano za ukanda chini ambapo wanapofanya utafiti wa mbegu wanaangalia mabadiliko ya tabia nchi ukinzani wa magonjwa na uongezaji tija kwa Wakulima .
Kwa upande wake kMratibu wa mafunzo ya sayansi na teknolojia kutoka Tume ya taifa ya sayansi na teknolojia (COSTECH ) Deusdedith Leonard amesema kuwa lengo la mafunzo hayo kwa wanahabari Ni kuhakikisha taarifa za sayansi zinaifikia jamii kwa ufasaha na kwa wakati.
Amesema kuwa wapo watafiti , ambao wametafiti vitu vikubwa lakini kutokana na kutokuwepo kwa taarifa sahihi jamii haipati taarifa hizo hivyo kupitia mafunzo hayo yatasaidia kuleta mabadiliko channya.