Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt.Herbert Makoye akizungumza na waandishi wa habari wakati akielezea mafanikio ya Taasisi hiyo ndani ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita Madarakani. Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt.Herbert Makoye akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati akielezea mafanikio ya Taasisi hiyo ndani ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita Madarakani
******************
NA EMMANUEL MBATILO, BAGAMOYO
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imeeleza mafanikio waliyoyapa katika kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita Madaraka.
Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati akieleza mafanikio hayo Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt.Herbert Makoye amesema mambo mengi yafanyika katika taasisi hiyo na yenye tija kwa jamii ambapo katika mwaka mmoja huo Taasisi imepata fedha ya Maendeleo kutoka serikalini kwa ajili ya ukarabati wa majengo kiasi cha shilingi Milioni 150 pamoja na ununuzi wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia kiasi cha shilingi milioni 100.
"Tumepata hiyo fedha tumeboresha miundombinu na tumeongeza miundombinu kwa maana hiyo pia hata udahili wa wanachuo umeongezeka kwasababu mwaka huu wa masomo 2021/22 tumedahiri takribani anachuo 695 lakini wale ambao wamefika na kujisajili ni 533 kulinganisha na huko nyuma ambapo kipindi ambacho tulidahili wanachuo wengi hawakuzidi 350". Amesema Dkt.Makoye
Amesema Royal Tour imechangia kwa kiasi kikubwa kuitangaza Taasisi hiyo ndani na nje ya nchi kwa kuwa TaSUBa ilikuwa moja ya sehemu ambazo utayarishaji wa documentary ya kutangaza nchi na vivutio vyake ilifanyika.
"Ndani ya mwaka huu mmoja tayari Rais ameshafika kwenye taasisi yetu katika zoezi la kurekodi filamu ya Royal Tour, kwa upande wetu tulifarijika sana kwasababu hii nchi ni kubwa lakini Rais aliona ni vyema kufika kwenye taasisi yetu". Amesema
Dkt.Makoye amesema Tamasha kubwa la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni lililofanyika Novemba, 2021 lilikuwa na mafanikio makubwa, lilivutia watazamaji takribani 70,000 kutoka ndani na nje ya nchi.
Aidha amesema katika Tamasha hilo la Sanaa na Utamaduni takribani vikundi 80 vya ndani ya nchi yetu vilikuja kushiriki na vingine vitano kutoka nje ya nchi virishiki , vilikuja vichache kutoka nje ya nchi kutokana na janga la Uviko 19.
Pamoja na hayo Dkt.Makoye amesema Taasisi hiyo inamategemeo makubwa kwasababu ukiangalia hata kwa upande wa fedha wanazoletewa kutoka serikalini nayo imeongezeka.
Social Plugin