Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TBS YAHIMIZA WASAFIRISHAJI WA BIDHAA NJE YA NCHI KUPIMA BIDHAA ZAO KABLA YA KUZISAFIRISHA

Afisa Udhibiti Ubora (TBS) Hassan Juma akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Makao Makuu ya TBS leo Jijini Dar es Salaam.

**************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) hutoa huduma ya msaada wa kitaalamu kwa wasafirishaji wa bidhaa nje ya nchi ili kusaidia wafanyabiashara kusafirisha bidhaa zilizokidhi matakwa ya viwango vya nchi husika.

Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na Afisa Udhibiti Ubora (TBS) Hassan Juma wakati akizungumza na wanahabari akielezea huduma hiyo.

Hassan amesema kwa nchi za Jumuiya ya Afrika mashariki bidhaa ambayo imethibitishwa na TBS huwa haina kipingamizi lakini zinazokwenda nje huwa wanatoa huduma za ukaguzi kabla ya kwenda nje sambamba na utoaji wa cheti.

‘Kwa bidhaa zinazokwenda nje ya jumuiya ya Afrika Mashariki huwa tunawapa taarifa ya nini kinahitajika kwa nchi husika kwa upande wa viwango kama mfanyabiashara atakua hana taarifa hizo vilevile huwa tunakaguana kuipima ubora wake kabla ya kuisafirisha na kutoa cheti.’amesema Hassan

Hassan ametoa wito kwa wafanyabiashara kutumia huduma hii kwani itawawezesha kusafirisha bidhaa zenye ubora na kuepuka usumbufu wa bidhaa kurudishwa nchini kwa kutokukidhi matakwa ya viwango.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com