TCCIA MWANZA YAKUTANA NA WANACHAMA WAKE KUPOKEA MAONI


Mwandishi wetu -Mwanza

Chemba ya wafanyabishara wenye viwanda na kilimo TCCIA Mkoa wa Mwanza imekutana na wanachama wake na kupokea maoni ya kuboresha utendaji kazi wake

Mwenyekiti wa TCCIA Mwanza Gabriel Mugimi ameiambia Malunde 1 Blog kuwa, dhamira ya kikao hicho ni kupokea maoni toka kwa wanachama wake ili kuweza kubaini changamoto mbalimbali zinazowakumba wafanyabishara na wakulima Mkoa wa Mwanza.

Mugimi aliongeza kuwa, kazi ya TCCIA ni kuhakikisha wanachama wake wanakuwa na elimu pana juu ya sheria zinazosimamia biashara na kilimo Nchini Tanzania kwani kujua sheria husika ni jambo la muhimu sana.

"Tuna imani kuwa, kupokea maoni na ushauri toka kwenu wanachama kutasaidia kuifanya taasisi yetu ya TCCIA kuwa imara na yenye nguvu",alisema.

Kwa upande wao washiriki wa mkutano huo waliibuka changamoto mbalimbali zikiwemo umuhimu wa elimu kwa wafanyabishara na maafisa wa mamlaka za serikali.

Justine Nelson kutoka taasisi ya Victoria Polybags alisema kuwa, kuna changamoto kubwa ya utozwaji wa kodi toka kwa maafisa wa TRA kwani inachangia kuua biashara badala ya kuendeleza.

Naye Bakari Kaoabi Mwenyekiti wa wavuvi ziwa Victoria alisema kuwa, baadhi ya sheria za uvuvi zinarudisha nyuma jitihada kukuza uchumi wa Nchi.

Pia alibainisha kuwa kuingiliana kwa wizara ndani ya sekta ya uvuvi kunarudisha nyuma jitihada za kukuza uvuvi Nchini hivyo ni vyema TCCIA Mkoa wa Mwanza ikaingilia kati.

Kikao hicho kilihusisha wanachama wa TCCIA wa Mkoa wa Mwanza na kimefanyika kwenye ukumbi wa Nyanza Jijini Mwanza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post