Kamishna Mkuu wa TRA ,Alphayo Kidata
Na Dotto Kwilasa,Malunde 1 Blog-DODOMA.
KATIKA kipindi cha mwezi Julai hadi Januari mwaka 2021-2022 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 12.937 sawa na ufanisi wa asilimia 96.8 ya lengo la kukusanya shilingi trilioni 13.370.
Hayo yameelezwa leo Machi 3,2022,Jijini hapa na Kamishna Mkuu wa TRA ,Alphayo Kidata wakati akizungumza katika uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo na kueleza kuwa kati ya kiasi hicho makusanyo halisi kwa Tanzania Bara ni shilingi trilioni 12.743 sawa na ufanisi wa asilimia 97.0 kutoka kwenye lengo la kukusanya shilingi trilioni 13.136.
Aidha kwa Zanzibar makusanyo halisi yakiwa ni shilingi 193,935.7 sawa na ufanisi wa asilimia 82.7 ukilinganisha na lengo la kukusanya shilingi milioni 234,573.9.
Kamishna huyo wa TRA amesema wastani wa makusanyo kwa mwezi katika mwaka wa kwanza wa shughuli za mamlaka hiyo mwaka 1996-1997 yalikuwa shilingi bilioni 42.
Amesema hivi sasa wastani wa makusanyo kwa mwezi ni shilingi trilioni 1.85 ambapo amedai kwa mwezi Disemba 2022 Mamlaka imefanikiwa kukusanya shilingi trilioni 2.5 ikiwa ni kiwango cha juu zaidi ya makusanyo yote ya mwezi tangu nchi ipate uhuru.
Kamishna huyo amesema katika kipindi cha mwezi Julai hadi Januari cha mwaka 2021-2022 imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 12.937 sawa na ufanisi wa asilimia 96.8 ya lengo la kukusanya shilingi trilioni 13.370.
Amesema kati ya kiasi hicho makusanyo halisi kwa Tanzania Bara ni shilingi trilioni 12.743 sawa na ufanisi wa asilimia 97.0 kutoka kwenye lengo la kukusanya shilingi trilioni 13.136.
Amesema kwa Zanzibar makusanyo halisi yakiwa ni shilingi 193,935.7 sawa na ufanisi wa asilimia 82.7 ukilinganisha na lengo la kukusanya shilingi milioni 234,573.9
Vilevile, amesema TRA imedhamiria kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa kuimarisha namna ya ukusanyaji wa mapato udhibiti wa mianya ya upotevu kodi,kubainisha vyanzo vipya vya mapato na kuweka mazingira rafiki kwa walipa kodi.
Kwa upande wake,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,Lawrence Mafuru ambaye alimwakilisha Naibu Waziri wa Wizara hiyo,Hamad Hassan Chande ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema baraza hilo lina wajibu kuwa chombo cha kufanya tathmini ya jinsi gani majukumu hayo yanatekelezwa kwa ufanisi.
Amesema ni wajibu wa baraza hilo kujitathmini ni jinsi gani wanaishauri Serikali katika masuala yote ili kujiridhisha kuwa ushauri wanaotoa unabeba maslahi mapana ya taifa na kuzingatia vipaumbele vya Serikali ya awamu ya sita.