Watumishi wanawake wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) wakiwa katika maandamano walipoungana na wanawake duniani kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa yamefanyika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma.
Watumishi wanawake wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) wakipita kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka wakati wa maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani yaliyofanyika leo March 08, 2022 ambapo kimkoa yamefanyika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma.
Watumishi wanawake wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) wakiwa katika maadhimisho ya picha ya pamoja mara baada ya kushiriki maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa yamefanyika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma.
Watumishi wanawake wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) wakiwa wamebeba vitu mbalimbali walivyotoa msaada wa wa chakula,mafuta,Pempers na sukari kwa watoto wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi katika Kituo cha Matumaini Jijini Dodoma ikiwa ni kuadhimisho siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa yamefanyika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma.
Watumishi wanawake wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) wakimsikiliza Mlezi wa kijiji cha matumaini SR Christina Phidelis walipotembelea na kutoa misaada ya vitu mbalimbali kwa watoto wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ikiwa ni kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa yamefanyika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma.
...........................................................
Na Alex Sonna_DODOMA
KATIKA kuadhimisha siku ya wanawake duniani Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) imetoa msaada wa chakula, mafuta, Pempers na sukari kwa watoto wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi katika Kituo cha Matumaini Jijini hapa huku ukitolewa wito kwa watanzania kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum. Akizungumza leo Machi 8,2022,Jijini hapa wakati wa utoaji wa msaada huo,Afisa Utawala kutoka (TCDC), Joyce Kato amesema wamechagua kupeleka msaada huo katika kijiji cha Matumaini kutokana na mahitaji ya watoto kuwa makubwa.
“Tumechagua kijiji cha Matumaini kwa kuwa sisi kila tunaposhiriki maadhimisho tunachagua kituo cha kwenda kutoa msaada, mwaka jana tulienda Buigiri lakini sasa hivi tumechagua Matumaini kwa sababu hawa wana mahitaji sana,” amesema.
Amesema nia ya dhati ya TCDC ni kuwasaidia watoto kwa kuwa wamekuwa wakipata changamoto mbalimbali.
“Wito wetu kwa Taasisi zingine tujitoe tukipata uwezo wa kusaidia tusaidie kwa sababu hawa watoto wanatuhitaji sisi,” amesema. Naye, Mjumbe wa Kamati ya TUGHE wanawake, Tatu Mwenda amesema kwa mwaka huu waliandaa maadhimisho haya ambapo lengo ni kusheherekea na wanawake ambapo amedai walipata ushirikiano mkubwa kutoka kwa mwajiri kuanzia katika mavazi,mpaka misaada.
“Lengo kubwa ni kutoa msaada kwa watoto wale tumepeleka pampers za watoto,mchele,maharage,sabuni sukari tumetumia milioni moja ambayo Sister alituomba lakini sisi kama wazazi tumeona kuna vifaa vina umuhimu,”amesema.
Mwenda ametoa wito kwa Serikali,Makampuni na Taasisi kuendelea kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum huku akiupongeza uongozi wa TCDC kwa kujitolea kuwasaidia watoto. Kwa upande wake,Sister wa Kituo hicho,amesema wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali lakini wamekuwa wakizitatua kwa baadhi ya watu,taasisi na Serikali kuwasaidia
Amesema watoto hawa wanaishi vizuri kwa sababu wanatumia dawa na wengine tayari wamemaliza chuo na wana kazi na hakuna kukata tamaa licha ya kwamba watoto hao ni yatima lakini wanaishi kifamilia.
“Wengine wenye moyo wa kujitolea wanakuja mtu na mme wake ambao pengine wameishakuwa na watoto wakubwa wanalea wale watoto yatima mnampa nyumba mnamgawia na watoto ili wapate malezi ya baba na mama na wanaenda mara moja kwa mwezi. “Kuna wengine wamekaa sana kuna wengine wana miaka 16 tangu wamekuja na familia yao ambapo familia yako unaiacha nyumbani ili kuwalea watoto hao,”amesema.
Amesema watoto wanaioshi katika kituo hicho wapo 147 ukiacha wale ambao wapo shule za Sekondari na Vyuo. Amesema kuna mtoto wa siku 18 ambaye aliletwa katika kituo hicho mara baada ya mama yake kupata kichaa na wamekuwa wakimuhudumia vizuri.
“Na mdogo kabisa ana siku 18 tangu amezaliwa ameletwa akiwa na siku nane, Mama yake anashida anakichaa alimtupa hivyo ndugu walishindwa jinsi ya kumsaidia wakaona Mama wampeleke Mirembe na mtoto wamlete hapa sisi hatuwezi kukataa,”amesema.