Mradi wa maji Gamasara -Tarime
Na Dinna Maningo, Tarime
WANANCHI wa mtaa wa Gamasara kata ya Nyandoto wilaya ya Tarime mkoa wa Mara wamepata huduma ya maji ya Bomba ambayo awali walichota maji kwenye kisima kilichoelezwa kuchimbwa kwa hisani ya watu wa Misri ambacho kilikauka na kusababisha watu kufuata maji yasiyo safi na salama katika mto Mori.
Wakizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutembelea miradi ya maji inayojengwa kwa fedha za serikali kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini(RUWASA),Diwani wa kata ya Nyandoto Sinda Sabega alisema kuwa maji ya bomba yameondoa adha ya ukosefu wa maji iliyowakumba wananchi wake;
"Kisima kilichimbwa kwa hisani ya watu wa Misri mwaka 2010 ila hawakuweka mtandao wa mambomba kilikuwa tu kisima cha kawaida,mradi ulisimama kwa miaka 8,mwaka 2017 serikali iliufufua na kuleta pesa aliyekuwa waziri wa maji wakati huo alikuja akakiona akaagiza wataalamu wakisafishe ili waone kina uwezo wa kutoa maji kiasi gani,awali kilitoa maji lita 6000 kwa saa baada ya chemichemi kuziba na baadae maji yalipungua hadi Lita 26,00. alitoa maelekezo na pesa zikaletwa kama,sijasahau nikama Milioni kati ya 300 au 400,akasema mradi ujengwe upya bomba ziwekwe,umeme na mashine yakusukuma maji kwenda kwenye tenki na kutandaza mabomba,2020 mradi ulikamilika nakuanza kutoa maji", alisema Sabega
"Waziri wa maji Aweso naye alishakuja akaona,chanzo cha maji lakini ikaonekana kina uwezo mdogo wa kuhudumia mitaa yote akaagza kisima kingine kichimbwe kiongeze nguvu kimechimbwa bado hakijawekewa mtandao wa maji ili kianze kusambaza maji" alisema Sabega
Mwenyekiti wa Jumuiya ya watumiaji wa maji (CBWSO) Raheli Onyango alisema kuwa kabla ya mradi huo wananchi walikuwa wanachota maji mto Mori maji ambayo si safi na salama nakwamba huduma hiyo ya maji gharama yake ni sh 50 kwa ndoo moja inayochotwa.
Onyango alisema pesa zinazokusanywa uzihifadhi benk ambapo tayali wana kiasi cha zaidi ya laki nane ambazo bado hazijaanza kutumika kama vile kulipa umeme na matengenezo mengine ya mradi.
"Tulikuwa tunaamka saa 10 alfajiri tunatafuta maji tunaacha watoto majumbani,sasa maji yanapatikana na watu 47 wameunganishiwa maji majumbani,RUWASA wametupatia elimu ya umuhimu wa kutumia maji ya bomba ambayo ni safi na salama,kabla ya elimu watu walikuwa wanaacha maji ya Bomba wanaenda kuchota maji mto Mori,wengine bado hawachoti kisa maji ni ya kulipia". alisema Raheli.
Social Plugin