Mhadhiri msaidizi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Bw. Dunstan Haule akitoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Mugabe. Bw. Dunstan Haule mhadhiri msaidizi (mtaalam wa Uraibu) akijibu swali la mwanafunzi wa shule ya sekondari Mugabe wakati akioa elimu katika kuadhimisha siku ya Mwanamke Duniani. Wahadhiri wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Mkuu wa shule ya sekondari Mugabe na wanafunzi katika picha ya pamoja. Wanafunzi wa shule ya sekondari Mugabe walio katika kundirika wakisikiliza kwa makini elimu wanayopewa na Wahadhiri wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii. Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt. Joyce Nyoni akiwa amempakata mtoto wa kituo cha Kulea watoto yatima Faraja Mburahati. Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt. Joyce Nyoni akipokea risala kutoka kwa mwakilishi kituo cha Faraja Mburahati.
Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt Joyce Nyoni akikabidhi msaada wa mahitaji yaliyotolewa na Wanawake wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii kwa Mkurugenzi wa kituo cha kulea watoto Faraja Mburahati Bi. Zamda Idrisa Juma Jijini Dar es Salaam.
********************
Katika kuadhimisha ya siku ya Wanawake Duniani,Wanawake watumishi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii iliyo chini ya Wizara ya Maendeleo ya jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu kupitia kituo chake cha elimu,ushauri na msaada wa kisaikolojia wametembelea shule ya sekondari Mugabe na shule ya msingi mapambano kwa ajili ya kutoa elimu kwa wanafunzi juu ya mahusiano,maadili na uraibu wa madawa yakulevya na vilevi kwa kundi rika iliyotolewa na wahadhilri wa taasisi ya ustawi wa jamii.
Wakiongea katika nyakati tofauti tofauti mratibu wa kituo hicho Rufina Khumbe na mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari Mugabe Mwl.Mathew Mchome wamesema wamekuwa na changamoto za kitabia za mahusiano ya kimapenzi na utumiaji wa vilevi kwa vijana walio mashuleni hivyo kupelekea wanafunzi hawa kupata mimba zisizo tarajiwa na kuwa waraibu wa pombe na dawa za kulevya na kupelekea wanafunzi kusimama masomo au kuacha kabisa.
Wameeleza kuwa hata familia zinamchango mkubwa katika malezi ya wanafunzi na mazingira yanayo wazunguka katika kubadili tabia ya wanafunzi na hvyo kuomba Taasisi ya Ustawi wa Jamii kufika shule nyingi zaidi kuwasaidia wanafaunzi kupata Elimu sahihi na kuepuka makundi rika ili kutimiza ndoto zao.
Vilevile wanawake wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii walitembelea pia kituo cha Watoto yatima na Watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Faraja kilichopo Mburahati, Dar es salaam. Waliongozwa na Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt. Joyce Nyoni, ambapo walitoa msaada wa vitu mbalimbali ambavyo vitasaidia kituoni hapo.
Akiongea katika makabidhiano ya vitu hivyo Dkt. Nyoni amesema “Tungependa kuona ustawi mzuri wa Watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu wakipata huduma zote ambazo Watoto wengine wanapata ndio maana sisi kama Taasisi ya Ustawi wa Jamii na hasa wanawake tumewaletea kitu kidogo kama shukrani yetu kwenu kwa kuwalea Watoto hawa".
Naye mkurugenzi wa kituo cha Faraja Bi Zamda Idrisa Juma ameshukuru wanawake wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii kwa kutembelea kituo hicho. “Tumefurahi sana kutembelewa nanyi pia tunashukuru sana kwa msaada mliotupatia siku ya leo Mwenyezi Mungu awabariki na akawaongezee pale mlipo toa”amesema Bi Zamda.
Social Plugin