WAZIRI KADUARA AWATAKA WATUMISHI WIZARA YA MAJI, NISHATI NA MADINI KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO


Na Doreen Aloyce , Zanzibar
Waziri wa Maji,Nishati na Madini Shahibu Hassan Kaduara Visiwani Zanzibar amewataka watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano na juhudi kubwa pamoja na kusimamia nidhamu za watendaji wenzao jambo ambalo litasaidia kupiga hatua zaidi.

Kauli hiyo aliitoa Visiwani Zanzibar wakati wa makabidhiano ya Ofisi baina yake na Waziri aliyekuwepo kwenye Wizara hiyo Suleiman Masoud Makame baada ya kupangiwa Wizara ya Uchumi wa Blue na Uvuvi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi. 

Aidha Waziri Kaduara amesema kuwa hakuna jambo jema kama mashirikiano na kama  watazungumza lugha moja,nia moja  kazi itakuwa rahisi na badala ya kutawanyikana lengo la Serikali halitafikia.

"Leo nimekabidhiwa Ofsi mpya ninachowaahidi ni ushirikiano uliotukuka kikubwa tuendeleze pale tulipoachiwa na Waziri ambaye amemaliza muda wake na amefanya kazi nzuri ili wananchi wetu waone faida".

"Pia niwaombe mkasimamie nidhamu ya Wataalamu wenzetu tusiende kufukuza mtu,wala hakuna atakayefukuzwa na hakuna tutakayemuacha  bali turekebishe tabia zetu ili kujenga ufanisi uliotukuka tukifanya hivyo tutakuwa wamoja na kufurahia keki hii ambayo tumepewa", amesema Kaduara.

Naye Waziri aliyekuwepo awali ambaye amehamishiwa Wizara ya Uchumi wa Blue na Uvuvi Suleiman Masoud Makame amewaomba watumishi kufanya kazi kwa Umoja na kwamba yupo tayari kutoa ushirikiano,ushauri na maoni pale atakapotakiwa.

"Mimi niko tayari kufanya kazi naye  lile nililoanza nalo na nilipofikia ili tuweze kufikia adhma ya Serikali , na nimemkabidhi mambo mbalimbali Wizara na mashirika yake ikiwemo miradi inayoendelea mikubwa na ujenzi wa matanki "amesema Waziri Suleiman Masoud Makame .

Naibu waziri wa Wizara hiyo Shabani Ally Othuman amesema kuwa yale yote yaliyotolewa na Waziri yatatekelezwa kwa ufanisi ili kazi iweze kusonga mbele.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم