Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali (kulia) na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya DP World ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bandari, Bohari na Eneo Huru la Kibiashara – Dubai, Sultan Ahmed Bin Sulayem (kushoto) wakiwa katika zoezi la kutia saini hati za makubaliano ya ushirikiano kuendeleza miundombinu ya kupokea na kuhifadhia mafuta na gesi itakayojengwa nchini Tanzania.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali (kulia) na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya DP World ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bandari, Bohari na Eneo Huru la Kibiashara – Dubai, Sultan Ahmed Bin Sulayem (kushoto) wakipongezana mara baada ya kutia saini hati za makubaliano ya ushirikiano kuendeleza miundombinu ya kupokea na kuhifadhia mafuta na gesi itakayojengwa nchini Tanzania.
**********************
Wizara ya Nishati na kampuni ya DP World ya Dubai zimesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano katika kuendeleza miundombinu ya kupokea na kuhifadhia mafuta na gesi itakayojengwa nchini Tanzania.
Utiaji saini huo umefanywa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya DP World ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bandari, Bohari na Eneo Huru la Kibiashara – Dubai, Sultan Ahmed Bin Sulayem.
Mradi uliolengwa katika Hati ya Makubaliano husika ni kuendeleza miundombinu ya kitaifa iliyo bora na ya kisasa ya kupokea na kuhifadhi mafuta na gesi ambayo itatumika katika kuboresha sekta ya mafuta na gesi nchini na katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki.
Tukio hili lilifanyika tarehe 27 Februari, 2022 katika Kikao cha Kibiashara kilichofanyika huko Dubai – Umoja wa Falme za Kiarabu.
Social Plugin