Gari aina ya Coaster T 833 lililopata ajali wilayani Korogwe mkoani Tanga
**
WATU sita wamepoteza maisha na wengine 19 wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka wilayani Korogwe, mkoani Tanga.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Safia Jongo amesema ajali hiyo imetokea eneo la Kwamdulu ambapo gari aina ya Coaster yenye namba za usajili T833 DMH kuacha na kupinduka usiku wa kuamkia leo Jumanne Aprili 12, 2022.
“Waliofariki ni wanawake watatu na wanaume watatu ambapo katika hao wanawake, mmoja ni mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka mitatu na kati ya hizo maiti tano zimetambuliwa na ndugu zao huku mmoja bado hajataambuliwa,” amesema Kamanda Jongo.
Aidha, chanzo cha ajali hiyo kimeelezwa kuwa ni mwendokasi wa gari aina ya Coaster, ambalo lilimshinda dereva ndipo likaacha njia na kupinduka.
Social Plugin