Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAFULILA AIAGIZA TAKUKURU KUCHUNGUZA VYAMA VYA USHIRIKA


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu David Kafulila akiongea na wadau wa zao la Pamba mkoani Simiyu.

Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.

MKUU wa Mkoa wa Simiyu David Kafulila ameitaka Taasisi ya Kupambana na Kuziua Rushwa Mkoani humo kuhakikisha wanakamilisha uchunguzi juu vyama vya ushirika ambavyo vilipokea fedha na kuwalipa wakulima ili kujiridhisha kama malipo hayo ni sahihi.

Kafulila ameyasema hayo leo (Aprili 20,2022) kwenye mkutano wa kujadili tathimini ya zao la pamba kilichofanyika katika ukumbi wa Bariadi Conference na kuwakutanisha wadau wa pamba mkoani humo.

‘’Nataka nione kama Amcos zimewalipa wakulima kulingana na fedha walizopokea toka kwenye makampuni ya ununuzi wa pamba, tusiache jiwe juu ya jiwe, tusiache mtu hata mmoja aliyekula fedha za mkulima’’, amesema Kafulila.


Hata hivyo Kafulila ameshangazwa kuona Taasisi hiyo haijafanya uchunguzi tangu alipotoa maagizo jambo ambalo amesema limesikitisha sana, na kwamba ameitaka TAKUKURU kufanya uchunguzi huo haraka na aipate ripoti hiyo.


Aidha Kafulila amesema baadhi ya viongozi wa vyama vya Ushirika bado wanawaibia wakulima kupitia vyama vya ushirika ambapo si lengo la serikali kuwaibia wakulima kupitia ushirika.


‘’Tunataka kuona Mnunuzi hamwibii mkulima, Mkulima anataka bei stahiki na mnunuzi anataka kutoa bei stahiki…’’ amesema Kafulila.

Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba Marco Mtunga amesema mkoa wa Simiyu ndio wazalishaji wakubwa wa pamba nchini na kwamba changamoto nyingi za zao la pamba ziko mkoa wa Simiyu.


Alisema viongozi wa Amcos hawaambii wakulima juu ya mabadiliko ya bei, wanalipwa fedha kidogo wakati makampuni yanatoa bei kubwa kwa wakulima.


‘’kuna genge linagawana fedha za wakulima, ushirika mlitakiwa kufanya vizuri ili wakulima wapate fedha zao, ushirika mnawaibia wakulima ndio maana haiutaki ushirika’’ amesema Mtunga.


Alisema kuna Usimamizi mbovu sana kutoka kwa viongozi wa vyama vya ushirika, ambapo aliwataka kufanya vizuri ili kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi.


‘’Msitumie ilani kuharibu mambo ya watu, Ushirika ni Ilani, hata kama mnafanya vibata tung’anga’ane tu na ushirikia…’’ amesema Mtunga.


Gilang’hinda Busiga kutoka Kampuni ya Lugeye kutoka Mwanza, aliomba wafuate mfumo wa Amcos kuajiri wapimaji kulingana na makampuni yaliyofika kwenye Amcos, waajiri wahasibu ili kila kampuni liwe na mlango wake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com