Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NAPE NNAUYE AANZA ZIARA KUKAGUA UTEKELEZAJI NA KUHAMASISHA ZOEZI LA ANWANI ZA MAKAZI

 

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akiongea na Waandishi wa habari katika uwanja wa ndege jijini Dodoma kabla ya kuanza ziara yake ya kuzunguka nchini  kufanya uhamasishaji wa uwekaji anuani za makazi.
****


Na Dotto Kwilasa Malunde 1 blog- DODOMA

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye  ameanza ziara ya siku moja ya kukagua utekelezaji na kuhamasisha zoezi la Anwani za Makazi katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha huku akiitaka mikoa ya Tanga na Dar es Salaam kushindwa kufanya vizuri kwenye uwekaji wa anuani za makazi.

Hayo yamejiri  leo Jumatatu April 11, 2022 akiwa katika uwanja wa ndege jijini Dodoma wakati akianza ziara ya kuzunguka nchi nzima kufanya uhamasishaji wa uwekaji anuani za makazi kutimiza lengo la Serikali la  kuhakikisha kunakuwepo na anwani za kitaifa ambazo zitaainisha makazi, mahali zilipo Ofisi  na maeneo ya biashara.

Amesema shughuli hiyo ya uwekaji wa anuani za makazi nchini inatakiwa kuhitimishwa Mei 22, 2022 ingawa kwa sasa imefikia wastani wa asilimia 68 kwa nchi nzima.

"Tunafanya jitihada Kwenye sehemu zoezi hili linakotekelezwa ili kusaidia kuongeza utaalamu  katika mikoa yenye changamoto ya utekelezaji, lakini pia kuangalia sababu zilizosaidia mikoa mingine kufanikiwa zaidi na hivyo kuzitumia kusaidia mikoa ambayo inahitaji msaada zaidi”, amesema Waziri huyo.

"Operesheni hii iliyozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania   Samia Suluhu Hassan ambayo kwa sasa imefikia takribani asilimia 69 ina lengo la kuhakikisha kila Mtanzania anapata Anwani za Makazi ili kurahisisha  ufikishaji wa  huduma mbalimbali za  jamii na biashara kwa walengwa”, amesema.

Waziri huyo akiwa na timu yake wameanzia ziara hiyo mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha amesema katika baadhi ya maeneo wanalazimika kuongeza nguvu kupeleka wataalamu zaidi.

"Licha ya kuwa zoezi hilo limefanikiwa katika baadhi ya mikoa kama Lindi na Ruvuma bado kumekuwepo na mikoa michache ya Tanga na Dar es Salaam ambayo haijafanya vizuri na hivyo Serikali inajipanga kuhakikisha mikoa yote inafanikiwa katika zoezi hilo,"amesisitiza

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com