BIKIRA MWENYE MIAKA 70 ATAMANI MME.... ASEMA 'HAJAWAHI KULALA NA MWANAUME, HAJUI HATA INAKUWAJE!'


Mwanamke mwenye umri wa miaka 70, Verena, ambaye amekataliwa kimapenzi anasema hajakata tamaa na ana matumaini atakutana na mwanaume wake.

Akizungumza na AfriMax English, Verena, ambaye ni bikira, alifichua kwamba ni mtu aliyejawa upendo siku zote na hajawahi bahatika kukutana na mwanaume ampendaye. 

Alidai kuwa huenda hajapata mwanaume kwa sababu ya maumbile yake ya kimo kifupi akieleza kuwa hana ujasiri wa kukaribia au kuzungumza na wanaume.

"Mimi bado ni bikira. Sijawahi kuolewa, sijawahi kulala na mwanaume na sijui inakuwaje," alisema.

Akiongeza kuwa: "Bado nina matumaini ya kupata mpenzi."

Verena alisema anatumai kupatana na mahabubu wake na kuolewa, akifichua kwamba siku zote alikuwa akitamani kuingia katika ndoa baada ya kufikisha miaka 20, lakini anahofia kwamba anaweza kufa kabla ya kukutana na mpenziwe. 

Alifichua kuwa hajawahi kukutana au kulala na mwanaume katika maisha yake yote na anaendelea kujiweka kwa ajili ya mume wake.

 "Ninaishi maisha ya uchungu kwa sababu huwa naumwa kila mara. Ninakosa pesa za matibabu..." 

Katika taarifa sawia na hiyo, mwanamke mwenye umri wa miaka 70 ambaye hajawahi kuwa katika uhusiano au kulala na mwanamume yeyote alisema kuwa anamtafuta mwanamume ambaye ana umri wa miaka 21.

Genevieve, kama anavyofahamika, ana changamoto ya kiafya inayomlazimu kutambaa kwani hawezi kutumia miguu yake. Bikizee huyo mwenye umri wa miaka 70, amekuwa akiishi pekee yake baada ya wazazi wake kufariki, na majirani zake hujitolea kumpa msaada anaohitaji.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم