Waziri Wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ametoa Cheti cha Pongezi kwa Shirika la Wekeza kwa Mtoto na Kuimarisha Familia ICS la Mjini Shinyanga linalo tekeleza Miradi ya Kijamii katika Kupinga Ukatili wa Wanawake na Watoto Kupitia Utoaji wa Elimu ya Malezi na Makuzi Bora kwa Mtoto Baada ya kufanikiwa Kuanzisha Mfumo wa Elimu kwa Njia ya Mtandao kwa kutumia Simu Janja kwa lengo la kuhamasisha jamii itambue umuhimu wa Malezi Bora kwa Ustawi wa Watoto.
Aidha wengine waliopata vyeti vya pongezi ni pamoja na taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR),Chuo Kikuu cha Oxford Uingereza , Chuo Kikuu cha Cape Town Afrika Kusini CWBSA, IDEMS INTERNATIONAL,Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga,Tedson Ngwale pamoja na Afisa Ustawi wa Mkoa huo Bi. Lidia Kwesigabo kwa mshikamamo na uongozi mzuri wa wadau uliofanikisha kudhibiti mauaji ya kinyama kwa Wazee kutokana na imani potofu za kishirikina kuwa kila mzee mwenye Macho Mekundu eti ni Mchawi.
Dkt. Gwajima amesema kuwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalumu ina mpango wa Kuanzisha Tuzo ya Siku ya Mashujaa wa Mapinduzi ya Kutokomeza Ukatili kwa Wanawake, Watoto na Wazee ili kuongeza hamasa kwa Jamii inayoshiriki kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia hapa nchini.
Kwa Upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu- (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) ambaye Pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi amesema kuwa Jamii inapaswa Kubadilika kuwa na Malezi bora kwa watoto ili kujenga Taifa lenye maadili mema
Mkurugenzi wa Shirika la ICS Kudely Sokoine amesema Shirika lina mpango wa kufikia watu laki sita (600,000) katika Mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Kilimanjaro na Simiyu kwa lengo la Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.
Soma pia:
Waziri Wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza leo Jumapili Aprili 24,2022 katika ofisi za Shirika la Wekeza kwa Mtoto na Kuimarisha Familia (ICS la Mjini Shinyanga.
Waziri Wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza leo Jumapili Aprili 24,2022 katika ofisi za Shirika la Wekeza kwa Mtoto na Kuimarisha Familia (ICS la Mjini Shinyanga.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) ambaye Pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi akizungumza katika ofisi za Shirika la ICS wakati Waziri Wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima alipotembelea shirika la ICS leo Jumapili Aprili 24,2022
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu akizungumza katika ofisi za Shirika la ICS wakati Waziri Wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima alipotembelea shirika la ICS leo Jumapili Aprili 24,2022
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza katika ofisi za Shirika la ICS wakati Waziri Wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima alipotembelea shirika la ICS leo Jumapili Aprili 24,2022
Social Plugin