Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI KATAMBI ALA PASAKA NA WATU WENYE ULEMAVU DODOMA


Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu Wizara ya kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu ambaye pia ni Mbunge Shinyanga mjini leo Aprili 17, 2022 ,Sikukuu ya Pasaka amekula chakula na watu wenye ulemavu katika kituo cha Samaria kilichopo kata ya Hombolo Dodoma.

Kituo cha Samaria kilichopo kata ya Hombolo ni moja ya kituo kinachotoa huduma kwa watu wenye ulemavu,wazee, wenye ukoma na ugonjwa wa macho.

Hata hivyo mhe. Katambi ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuwapunguzia changamoto za kimaisha,miundombinu kama sehemu ya idara katika Wizara yake


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com