Mwanaume mmoja anashikiliwa na Polisi kwa kumdunga kisu hadi kufa kakaake katika kaunti ya Kakamega nchini Kenya.
Kisa hicho kilichofanyika katika kijiji cha Senyende kaunti ya Kakamega ambapo mwanaume Bonaventure Lumwachi, 37, amemdunga kisu hadi kufa kakaake mdogo Augustine, 35, baada ya ugomvi kuhusu kuku aliyepotea.
Ndugu zao walisema mshtakiwa alimvamia kaka yake na kumchoma kisu chenye ncha kali kifuani baada ya ugomvi wa mahali alipo kuku huyo.
Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha eneo hilo.
Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Shinyalu Robert Makau alisema wanakijiji waliokuwa na hasira walimvamia mshukiwa wa mauaji hayo kabla ya kuokolewa na kupelekwa hospitalini.
Hivyo amelazwa katika hospitali kuu ya kaunti ya Kakamega akiwa katika hali mahututi.
“Mshukiwa anaendelea kupokea matibabu katika Hospitali Kuu ya Kaunti ya Kakamega. Atashtakiwa kwa mauaji mara tu atakaporuhusiwa kutoka hospitalini,alisema Makau.
Social Plugin