KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, ameshiriki maziko ya Msanii Maunda Zorro, yaliyofanyika Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam leo Aprili 16, 2022.
Katika maziko hayo, Shaka alijumuika na wanafamilia na waombolezaji, ndugu jamaa na marafiki ambapo alipata nafasi ya kuwasilisha salamu za pole na mkono wa rambirambi kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
”Mhe Rais Samia yuko safari (ziara) amenituma nifikishe salamu zake za pole kwenu ndugu, familia, jamaa na marafiki sambamba na kuwasilisha mkono wa rambi rambi toka kwake, anatambua kuwa tasnia hii imepoteza msanii mahiri ambaye wakati wote wa uhai wake aliitumia sanaa kufikisha ujumbe.
"Kuburudisha, kuhamasisha na wakati mwingine kuiunganisha jamii kwa ujumbe, sambamba na kuenzi kipaji cha (baba yake) Mzee Zahiri Zorro, lakini Maunda akiwa msanii anayechipukia alifanya vizuri sana,”amesema Shaka katika sehemu ya maelezo yake.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe, Apumzike kwa Amani Maunda Zorro. Ameen.
Social Plugin