Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akizungumza katika ziara yake ya kukagua zoezi la anwani za makazi mkoani Arusha katika eneo la shule ya msingi Ngarenaro jijini humo.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akizungumza katika ziara yake ya kukagua zoezi la anwani za makazi mkoani Arusha katika eneo la shule ya msingi Ngarenaro jijini humo.
Na Agness Nyamaru, Arusha.
Waziri wa habari,maasiliano na Teknolojia ya habari,Nape Nnauye amewataka wananchi kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali mkoani Arusha kutumia zoezi la anwani za makazi kuwaenzi waasisi na wabunifu ili kulinda historia yao.
Waziri Nape aliyasema hayo leo Jumanne Aprili 12,2022 wakati wa ziara yake ya kukagua zoezi la anwani za makazi mkoani Arusha ambapo ameelekeza kuangalia njia ya kutumia zoezi hilo kuenzi historia ya nchi kwa kutaja majina ya viongozi na wabunifu katika maeneo yao ya mitaa na barabara kubwa kutokana na utendaji kazi wao katika kutengeneza historia ya nchi.
Amesema wanaiingiza Tanzania kwenye nchi zenye ustaarabu wa kuweza kuhudumiana kistarabu maana bila anwani hatutaweza kutafutana lakini kwa anwani huduma nyingi zitaboreshwa na historia ya wote waliohusika kwenye jambo hilo wataitengeneza vizuri ili wakumbukwe katika kubadilisha maisha ya watu.
Mfumo huo ni wamuhimu sana ndio maana wanapambana kimamilisha kimamilifu zoezi hilo mnamo tarehe 22/5 mwaka huu ili liwe tayari,maana ni kazi iliyotangazwa na rais hakuna kushidwa kwa gharama yoyote ile.
"Tumekuja Arusha kukagua na kuona zoezi hili linaendeleaje mimi na wenzangu tunafuraha kubwa katika mikoa inayofanya vizuri,mkoa wa Arusha ni mkoa miongoni mwao unaofanya vizuri sana kwenye zoezi hili,"amesema Waziri Nape.
Mkoa wa Arusha ni mkoa ambao umekuwa na ubunifu wa kipekee ikiwa gharama za kuweka nguzo ni kubwa kutokana na asili yake,na viongozi wote wa mkoa huo wamefanikiwa kusimamia ubunifu wa kutengeneza kambi kwa ajili ya kutengeneza vifaa vya anwani za makazi.
Waziri Nape amesema mfumo huo ukikamilika utabadilisha hali ya nchi ya Tanzania,huku akibainisha kuwa Arusha ni moja ya mikoa na majiji yatakayofaidika sana na shughuli za utalii, ikiwa zoezi hili litasaidia kuboresha shunguli hizo kwenye eneo husika.
"Tunafurahia uzalendo wenu na mahali ambapo huu mfumo umefanyika vizuri ni kwa wajanja,Arusha mmeingia kwenye orodha ya wajanja katika nchi hii maana kuwa na anwani za makazi ni ujanja na kutokuwa na anwani za makazi ni ushamba,"amepongeza Waziri huyo.
Aidha Waziri Nape amewaagiza Wakala wa barabara mijini(TANROADS) na wakala wa barabara vijijini (Tarura) kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo ili liweze kukamilika kwa wakati.
Naye Mkuu wa mkoa wa Arusha,John Mongella amesema zoezi hilo mkoani hapo linatarajiwa kukamilika mnamo Aprili 30,2022 hivyo wataongeza juhudi na umakini katika kukamilisha kwa wakati.
Katibu tawala Msaidizi wa mkoa wa Arusha,Said Mabiye amesema mkoa wa Arusha umeshapokea takribani sh.milioni 905.1 kwa ajili ya halmashauri zote kuweza kutekeleza zoezi hilo na anuani za makazi.
Amesema katika zoezi hilo Jiji la Arusha limefikia katika hatua ya asilimia 78.72, halmashauri ya Monduli asilimia 45.82,Longido asilimia 39.04, Ngorongoro asilimia 12.51,Arusha asilimia 11.21,Meru asilimia 4.21 na Karatu ni asilimia 2.
Social Plugin