Na John Walter-Babati
Mtoto wa kiume anaekadiriwa kuwa na umri wa miezi 8-9 ametupwa na mtu ambaye hadi sasa hajafahamika katika kitongoji cha Dulaqang' kijiji cha Sabilo kata ya Dabil wilayani Babati kisha kuokotwa mbwa.
Mtoto huyo amekutwa tayari amefariki dunia huku kichwa na mkono vikiwa vimeondolewa.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kijiji cha Sabilo Arkadi Moshi, mtoto huyo alitupwa kwenye eneo la chanzo cha maji kilichopo kijijini hapo.
Tukio hilo limetokea Aprili 4,2022 majira ya saa 12 jioni katika barabara ya Dareda-Gitting ambapo walibaini kisa hicho baada ya kumuona mbwa akiwa amebeba kiwiliwili ambacho katika kufuatilia waligundua kuwa ni cha binadamu ndipo wakamfukuza mbwa huyo na kuchukua mwili huo na kuuhifadhi pembezoni mwa barabara.
Ameeleza baadaye wananchi waliitana kwa kupiga yowe na kukusanyika ili kufuatilia ili kumtambua aliyefanya kitendo hicho na mpaka sasa jitihada za kumtafuta zinaendelea ambapo mkutano maalum wa kijiji umeitishwa.
Social Plugin