Josiah Mwesigye mwenye miaka 83, raia wa Uganda amefanikiwa kupata mtoto wake wa kwanza baada ya kutafuta mtoto bila mafanikio kwa miaka 57.
Josiah amepata mtoto wake wa kwanza na mke wake wa sasa Sharon Arinaitwe mwenye miaka 29 baada ya kufiwa na mke wake aliyekuwa na umri wa miaka 79 ambaye hakuacha mtoto.
Mzee huyo alizaliwa Januari 26, 1939, katika Kitongoji cha Bugangari, Wilaya ya Rukungiri nchini Uganda ambapo akiwa na miaka 23, alifunga ndoa na Jane Tukamuhabwa ambaye sasa marehemu Aprili 25, 1962.
Mwesigye alisubiri kwa miaka 57 ya ndoa yake bila mafanikio ya kupata mtoto hadi mke wake alipofariki
Social Plugin