Watu wawili wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi katika kijiji cha Idiwili ,Mbozi mkoani Songwe leo jioni ya Aprili 6, 2022.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Idiwili, Carolina Kikoti amethibitisha kutokea tukio hilo na kueleza kuwa radi hiyo iliwapiga wakiwa shambani.
Amewataja waliofariki dunia kuwa ni Stenala Mwambongoro (54) na mtoto wake Raheli Msongole (16) wakati majeruhi ni Sephania Mwasenga na Tabia Haonga majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika kituo cha Iyula kilichopo Mbozi Songwe.
Chanzo : https://www.instagram.com/p/CcA2eKUtFzY/?utm_medium=copy_link
Social Plugin