

Dodoma 20 Aprili 2022 –Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Dkt. Tulia Ackson. Spika ameipongeza Benki ya CRDB kuuenzi mwezi Ramadhani kwa kuwa karibu na jamii katika kipindi cha mfungo wa Ramadhani. Spika ametoa pongezi hizo akipokea zawadi za mwezi wa Ramadhani kwa niaba ya wabunge ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa Benki ya CRDB kushirikiana na wateja wake na makundi mbalimbali katika jamii katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani. Zawadi hizo zilikabidhiwa katika Ofisi za Bunge na Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile.
Akizungumza wakati wa kupokea zawadi hizo Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson alisema kuwa Benki ya CRDB imekua mstari wa mbele kushirikiana na wadau na kuwataka kuendeleza utamaduni huo hata baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
“Nawapongeza sana Benki ya CRDB kwa kuendeleza utaratibu wao wa kuwa karibu na jamii katika kipindi hiki cha Mfungo wa Ramadhani na hasa kwa kugusa makundi mbalimbali hususani wahitaji na niwaombe waendeleze utaratibu huu hata baada ya mwezi Ramadhani” alisema Mh. Tulia

“Pamoja na kuwa leo tupo hapa kwa ajili ya waheshimiwa wabunge lakini tumeendeleza utaratibu wetu wa kufuturisha wateja wetu na makundi yenye mahitaji maalumu ambapo tangu tumeanza mwezi Ramadhani tayari tumeshafanya hivyo kwa mikoa ya Tanga na Shinyanga na wiki hii tunarajia kufanya hivyo kwa mikoa ya Mtwara, Njombe, Mwanza na pia tutafanya hivyo visiwani Zanzibar” aliongeza Bruce.
Pamoja na ushiriki katika mfungo wa mwezi Ramadhan kupitia futari na misaada kwa wenye uhitaji, hivi karibuni Benki ya CRDB imeanzisha huduma maalum za fedha inayozingatia misingi ya kutotoa na kupokea riba inayoitwa Al Barakah. Hadi sasa huduma ya Al Barakah imevutia wateja zaidi ya elfu nane huku mikopo iliyotolewa kupitia huduma hiyo ikiwa na thamani zaidi ya Shilingi Bilioni 8. 

Social Plugin