Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ULINZI WAIMARISHWA KUELEKEA UZINDUZI WA FILAMU YA THE ROYAL TOUR JIJINI ARUSHA


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishina Msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo.

Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishina Msaidizi wa Polisi ACP JUSTINE MASEJO amewaambia wananchi kuwa hali ya ulinzi na usalama katika jiji la Arusha na Mkoa ni shwari kuelekea uzinduzi wa filamu ya The Royal Tour.


Kamanda Masejo amesema kuwa kuelekea uzinduzi wa filamu maalum ya The Royal Tour Tanzania kuwa Jeshi la Polisi Mkoani humo limejianga vyema kuhakikisha dunia inashuhudia uzinduzi huo wa filamu ya the Royal Tour itakay fanyika siku ya kesho 28.04.2022 katika kituo cha kimataifa cha Mikutano Arusha AICC.


Kamanda Masejo amesema kama ilivyo desturi ya wakazi wa jiji la Arusha kuwa wakarimu kwa wageni basi vyema wakaionyesha dunia ukarimu huo na kuionyesha dunia kuwa Arusha ni kitovu cha utalii.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com