Khadija Seif na Humphrey Shao, Michuzi Tv
Kutoka katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere ambapo leo Aprili 2, 2021 kunafanyika hafla ya utoaji tuzo za muziki zilizoandaliwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia BASATA ambapo tukio limeanza kwa kutoa tuzo za heshima na tuzo maalum iliyotolewa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuthamini mchango wake mkubwa katika sekta ya sanaa nchini.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Matiko Mniko akizungumza na wadau wa Muziki na wageni waalikwa katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere katika hafla ya utoaji Tuzo ambapo tayari amegawa Tuzo za Heshima 4.
Mniko amemtaja Msanii wa Bongofleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond platinum Kwa kutambua Mchango wake katika Muziki wa Bongofleva na kuleta Mapinduzi makubwa na kupelekea Muziki wa Bongofleva Kimataifa na kushirikiana na wasanii mbalimbali wa Kimataifa.
Aidha, Miongoni mwa waliopokea Tuzo za heshima ni pamoja na Mkuu wa Majeshi CDF Jenerali Venance salvatory Mabeyo Kwa Mchango mkubwa uliofanyika katika Vita Vya Uganda na nyimbo nyingi kutungwa kipindi hiko ikiwa ni sehemu ya kuendelea kukuza Muziki nchini.

Social Plugin